• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KONGWA YAPONGEZWA KUPATA HATI SAFI KWA MIAKA SITA MFULULIZO

Imetumwa : July 9th, 2023


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule apongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kwa kupata Hati safi za Ukaguzi kwa hesabu zilizoishia tarehe 30 Juni, 2022 kwa miaka sita mfululizo tangu mwaka wa Fedha 2016/2017 hadi 2021/2022. Senyamule amesema Kitendo hiki kimeipa heshima kubwa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Mkoa wa Dodoma na nchi kwa ujumla.

Senyamule ameyasema hayo leo wakati wa Mkutano wa Baraza Maalumu la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kujadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2022/23. Amesema Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa ina jumla ya hoja 54 ambapo katika hoja hizo 39 ni za miaka ya nyuma na hoja 15 ni hoja za mwaka wa ukaguzi 2021/2022, ambapo kati ya hoja 54 hoja 16 zimeshafungwa hivyo kubakiwa na hoja 38.

Kufuatia hoja 38 zilizosalia, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Dkt. Omary Nkullo kuwasilisha kwake Mkakati wa ujibuji wa hoja hizo ifikapo tarehe 30/07/2023.

Amesema uwepo kwa hoja nyingi za Ukaguzi kila mwaka, ni kutokana na kuwepo kwa udhaifu mkubwa wa mifumo ya udhibiti wa ndani katika Halmashauri unaosababisha baadhi ya shughuli za Halmashauri kutekelezwa pasipo kuzingatia ipasavyo Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo mbalimbali iliyopo katika uendeshaji wake jambo ambalo huibua hoja zisizokuwa na lazima.

“Mkurugenzi hapa niagize watumishi wote waliochukua masurufu na hawajafanya marejesho kwa wakati warejeshe fedha hizo mapema iwezekanavyo” Senyamule ameagiza.

Senyamule pia amesisitiza agenda endelevu ya mazingira na kuwataka wana Kongwa kuendelea kukijanisha Dodoma, kuhamisha elimu kwa kukemea utoro kwa wanafunzi mashuleni pia kutoa msukumo wa agenda ya kilimo.

“Anzeni kuandaa vitalu vya miche ya miti katika maeneo yenu ili maelekezo ya Serikali ya kupatanda miti milioni moja na laki tano kwa kila Halmashauri yaweze kutimia. Pia, mkadhibiti utoro katika shule zetu, Serikali inajenga miundombinu hii ya shule kwa gharama kubwa hivyo tuna wajibu wa kuhakikisha watoto wanakwenda shule” Senyamule amesisitiza.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu ametoa rai kwa watumishi wote kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni za utumishi wa umma ili kuepuka hoja za ukaguzi ambazo zinaweza kuepukika.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Remidius Mwema amesema Wilaya yake imekamilisha kwa wakati ujenzi wa madarasa kupitia mradi wa boost ambapo wilaya ilipokea kiasi cha Shilingi Bilioni 1.3 kwa ajili ya ujenzi wa Shule 2, Vyumba vya madarasa 26, madarasa ya awali 2, darasa  la elimu maalumu 1 na matundu 18 ya vyoo.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.