• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KUKOSEKANA KWA USAWA, CHANZO CHA MAAMBUKIZI VVU

Imetumwa : March 1st, 2023

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene (MB) amesema kukosekana kwa usawa ni chanzo kikuu cha maambukizi ya Virusi vya Ukimwi. Simbachawene amesema hayo leo 01 Machi 2023 katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya kupinga ubaguzi Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 1 Machi ambapo mwaka huu yamefanyika Mkoa wa Dodoma kwenye ukumbi wa Hoteli ya Morena.

Amesema, Tanzania inaungana na Dunia kuadhimisha siku hii kwani ubaguzi katika jamii unasababisha kukosekana kwa usawa, unyanyasaji na ubaguzi vinaongeza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na kusisitiza kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya ubaguzi na unyanyasaji wa kijinsia. Wanawake walio katika ubaguzi wapo katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya VVU. Amesema Mhe. Simbachawene.

Simbachawene ametoa Rai kwa viongozi wa dini kuisaidia Serikali kuhubiri amani na upendo miongoni mwa jamii kwani wao ni nguzo muhimu inayoweza kukomesha ubaguzi na kupelekea kufikiwa kwa malengo ya Serikali ya kutokomeza unyanyapaa, unyanyasaji na ubaguzi ifikapo mwaka 2030.

Miongoni mwa wadau wakubwa wa siku hii ni Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) ambapo Kaimu Mkurugenzi wake Bw. Jumanne Isango amesema

“Unyanyapaa bado ni kikwazo ndani ya jamii na tunatarajia ifikapo mwaka 2030 kama yalivyo malengo ya Kimataifa, pasiwepo na vifo vitokanavyo na Ukimwi, pasiwe na ubaguzi wala unyanyapaa kwa waathirika wa Virusi vya Ukimwi. Sauti hii tunataka ifike mbali ili kuweza kumaliza kabisa tatizo hili” Amesema Bw. Isango

Hata hivyo, Bi Grace Mallya ambaye ni mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la kupambana na Ukimwi Duniani (UNAIDS), ambao pia ni wadau waliofanikisha maadhimisho haya amesema mwaka 2021 ulianzishwa mpango wa kupinga Ukimwi ulioainisha mikakati ya kuondoa Ukimwi Duniani na Tanzania ni miongoni mwa washirika wa mpango huo kwani tafiti zinaonyesha nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara zina maambukizi makubwa ya VVU hasa kwa vijana wenye umri wa miaka 14 hadi 21 na wengi hawatumii dawa za kufubaza virusi hivyo huku changamoto kubwa ikitajwa kuwa ni ubaguzi.

Siku ya Kimataifa ya kupambana na ubaguzi Duniani ilianza kuadhimishwa nchini Tanzania mwaka 2014 ikiwa na lengo kuu la kupinga ubaguzi kwa watu wenye VVU na makundi maalumu kwenye jamii na huandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu ikishirikiana na wadau mbalimbali kama vile UNAIDS, TACAIDS, PASADA, Save the Children, Baraza la watu wanaoishi na VVU (NACOPHA), watu wenye ulemavu na makundi mengine mengi katika jamii na kauli mbiu ya mwaka huu ni “Okoa maisha, usibague”

 

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.