• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

LISHE MASHULENI KUONDOA UTORO KWA WANAFUNZI

Imetumwa : February 9th, 2023

                      

LISHE MASHULENI KUONDOA UTORO KWA WANAFUNZI

Mkoa wa Dodoma umefanya kikao cha lishe kwa robo ya kwanza ya mwaka 2023 chini ya mwenyekiti wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Godwin Gondwe kikihudhuriwa na wajumbe wa kamati ya Lishe Mkoa akiwemo Katibu Tawala Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na wadau mbalimbali wa lishe Mkoa.

Kikao hicho kimejadili ajenda mbalimbali zinazohusu masuala ya lishe kwa wanafunzi mashuleni ambayo ndio imekua ajenda kuu katika kikao cha mwaka huu. Suala la lishe kwa wanafunzi limepewa kipaumbele  katika vikao vya Mkoa kwakuwa limebeba ustawi wa elimu kwa Mkoa kama anavyosisitiza Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatuma Mganga

“Suala la lishe ni mtambuka na linahusisha kila sekta. Msisitizo uliopo sasa ni lishe mashuleni kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula na hii itasaidia kupunguza utoro ambao ndio tunapambana nao kila wakati. Asilimia 27 ya watoto ndio wanapata chakula shuleni mpaka sasa. Tulishaweka azimio kila shule ilime kuhakikisha watoto wanapata chakula. Tuna wajibu wa kuwafundisha watoto kulima. Tunategemea kila shule itakua na hazina ya kutosha ya kutunzia chakula kwa mwaka mzima na hapo tutakua tumefanikiwa kudhibiti utoro mashuleni na kuinua kiwango cha taaluma” Amesema Dkt. Mganga

Hatahivyo, Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Bestie Magoma ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya lishe Mkoa amesema kuwa suala la lishe linahitaji ushirikiano mkubwa kati ya Mkoa na Halmashauri zake ili maazimio yanayowekwa kwenye vikao hivi yaweze kutekelezeka na kuleta tija.

“Halmashauri moja ikifanya vibaya ni Mkoa mzima na hakuna Mkoa bila Halmashauri, nitoe rai, tuendelee kushirikiana na kwa pamoja kwani tunaona maendeleo yanayopigwa sasa kwenye kupunguza udumavu na lishe inaonekana inakwenda kuboreka hivyo tuendelee kushirikiana” Amesema Dkt. Magoma

Akihitimisha kwa kutoa maazimio yaliyofikiwa na wajumbe wa kikao hicho, Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Godwin Gondwe, amesema.

“Kikao kiangalie viashiria vya lishe vilivyotolewa, elimu ya lishe iwe endelevu kwa kushirikisha viongozi wa ngazi zote, tusimamie mikakati ya watoto kupata chakula shuleni na kuimarisha miundombinu ya uvunaji maji ya mvua.  Mhe. Mkuu wa Mkoa atatembelea maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya vituo vya lishe, asilimia 7.1 ya uwiano wa urefu na uzito kwa watoto upungue kufikia asilimia 3 na siku 1000 ni muhimu kwa lishe ya mtoto” Mhe. Gondwe

Baaadhi ya ajenda nyingine zilizojadiliwa kwenye kikao hicho ni pamoja na kukosekana kwa miundombinu rafiki kwa ajili ya unyonyeshaji watoto wachanga, uwasilishwaji wa maeneo kwa ajili ya kuchimba mabwawa ya kuhifadhi maji, kukosekana kwa miradi midogo midogo katika mipango ya Halmashauri, baadhi ya jamii kukosa elimu ya masuala ya lishe, baadhi ya kaya kukosa bustani za mbogamboga, baadhi ya Halmashauri kutoshirikisha viongozi wa dini katika masuala ya lishe na baadhi ya Halmashauri kutoingiza kwa wakati taarifa za utoaji wa matone ya vitamin ‘A’ kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano wakati wa kampeni.

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.