• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yafana sana Mjini Dodoma Aprili 26, 2017

Imetumwa : April 26th, 2017

DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli , leo tarehe 26 Aprili 2017, ameongoza maelfu ya Watanzania katika sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kukagua gwaride la vikosi vya Ulinzi na usalama lililoandaliwa kwa heshima yake, Rais Magufuli amewahakikisia Watanzania kuwa yeye na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein wataendelea kuulinda Muungano kwa nguvu zao zote na kwamba atakayejaribu kuuvunja atavunjika yeye.

“Muungano ndio silaha yetu, Ni nguvu yetu, Mimi na mwenzangu Dkt. Shein tutaulinda Muungano kwa nguvu zote, Yeyote atakayejaribu kuuvunja atavunjika yeye” amesema Rais Magufuli.

Aidha Dkt. Magufuli amewataka Watanzania kuendelea kudumisha amani iliyopo nchini kwani amani ndio chachu ya maendeleo yanayopatikana nchini.

Rais Magufuli amesema Tanzania imeweza kufikisha miaka 53 ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar kwa sababu ya amani iliyopo nchini iliyowezesha kupatikana mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuunganisha mataifa yetu mawili na kuunda Taifa moja lenye nguvu.

Aidha amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umewezesha kupatikana mafanikio makubwa katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Mhe. Rais ametaja mafanikio mengine yaliyopatikana kutokana na Muungano ni kukua kwa uchumi na Kukabiliana na matatizo ya umaskini na ukosefu wa ajira, kuimarisha miundombinu ya usafiri wa anga, majini, reli na nchi kavu.

Aidha, Muungano umeimarisha na kuboresha upatikanaji wa huduma za jamii ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya shule na hospitali pamoja na kukua kwa demokrasia nchini.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanziba Maadhimisho ya Sherehe za Muungano zinafanyika Mkoani Dodoma Makao Makuu ya Serikali ikiwa ni ishara tosha kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi imedhamiria kwa dhati kuhakikisha Makao Makuu ya Serikali yanakuwa Dodoma.

“Niwahakikishie wana Dodoma na Watanzania kwa ujumla kwamba Serikali sasa tumefika Dodoma na hatutarudi tena, na kama tulivyoahidi mwaka 2020 Serikali yote itakuwa imehamia hapa” amesema Rais Magufuli.

Sherehe za miaka 53 ya Muungano zimehudhuria na Viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na wajane wa Viongozi Waasisi wa Muungano mke wa hayati Mwalimu Julius Nyerere Mama Maria Nyerere na hayati Abeid Aman Karume, Mama Shadya Karume, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Viongozi wa Chama na Serikali.

Kauli mbiu ya Sherehe za Muungano mwaka huu ni “Miaka 53 ya Muungano, Tuulinde na Kuuimarisha, Tupige Vita Dawa za Kulevya na Kufanya Kazi kwa Bidii”.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.