• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mafunzo ya Utengenezaji Tovuti za Mikoa na Halmashauri za Wilaya

Imetumwa : March 20th, 2017

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Rehema Madenge leo Machi 20, 2017 amefungua rasmi mkutano wa mafunzo ya Utengenezaji Tovuti za Mikoa na Halmashauri za Wilaya uliohusisha Mikoa saba na Halmashauri zake ikiwa ni Mkoa wa Dar es salaam, Pwani, Iringa, Singida, Manyara, Geita na wenyeji Dodoma.

Mafunzo hayo pia yanafanyika mikoa yote ya Tanzania Bara katika mikoa ya kanda mbalimbali ikiwa ni pamoja na kituo cha Mkoa wa Mbeya, Morogoro, Mtwara, Kigoma na tayari kanda ya ziwa afunzo yalishafanyika kwenye Mkoa wa Mwanza.

Katika ufunguzi wa Mafunzo hayo, Katibu Tawala Ndg Rehema Madenge amewataka Maafisa Habari wa Serikali kuhakikisha wanatoa taarifa sahihi na kwa wakati ili jamii izipate na kuzifanyia kazi  na kuongeza kuwa hiyo itaepusha taarifa zisizo za ukweli kusambaa kwa jamii.

Ndg. Madenge ameongeza kuwa, matarajio ya Serikali baada ya kukamilika kwa mafunzo hayo yanayotarajiwa kufikia mwisho Machi 27, 2017 ni kuona Mikoa yote na Halmashauri zote  nchini zitakuwa na tovuti zake na hiyo itasaidia kuiunganisha Serikali na jamii itapata taarifa za Serikali kwa ukaribu na urahisi zaidi.

Vilevile amebainisha kuwa Serikali inatarajia baada ya mafunzo hayo, Maafisa Habari wa Serikali za Mikoa na Halmashauri za Wilaya wataweza kufanya kazi zao kwa zaidi na kwa njia itayovutia jamii kusoma habari hizo.

Pia amesema kuwa Serikali inatambua kwa muda mrefu kumekuwa na changamoto ya utayarishaji na uendeshaji wa tovuti na utoaji wa taarifa kwa wakati kwa baadhi ya Mikoa na Halmashauri za Wilaya.

"Jamii inahaki ya kupata taarifa za shughuli za Serikali na haki hiyo ni kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" alibainisha Ndg. Madenge na kuongeza kuwa ni vema Maafisa Habari wa Serikali wakawa wanahakiki taarifa wanazozitoa kwa Umma kabla hawajazirusha hewani.

 Ndg. Madenge amewataka Maafisa Habari wa Serikali kutambua kuwa kukamilisha kutengeneza tovuti za Serikali za Mikoa na Halmashauri za Wilaya zitaongeza wigo wa dhana ya uwazi na uwajibikaji kwa wananchi wake kwa kuwajulisha mambo yote muhimu yanayotekelezwa na Serikali na hivyo amewataka kuhakikisha tovuti hizo zinawekwa taarifa mpya kila wakati na kumaliza utamaduni wa baadhi ya tovuti kuwa na taarifa za muda mrefu na zilizo pitwa na wakati. Baadhi ya Tovuti zina taarifa za mwaka jana hadi mwaka juzi.

Akizungumzia Malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano, amesema kuwa Serikali inalenga kuifanya nchi yetu kuwa ya viwanda na uchumi wa kati na sekta za kilimo na mifugo zikiwa na mchango mkubwa  katika kuilisha sekta ya viwanda hivyo kupitia tovuti hizo za serikali kuongeza kasi ya upashanaji habari za kilimo na mifugo.

Mafunzo hayo yatakayokamilika Machi 27, 2017, yanaendeshwa na kusimamiwa na Taasisi ya kuimarisha mifumo ya Umma (PS3) kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wakala ya Serikali Mtandao.

 

Imetolewa na:

Jeremia Mwakyoma

AFISA HABARI WA MKOA

OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA

Machi 20, 2017

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.