• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Makabidhiano Rasmi ya Ofisi kati ya Mkuu Mpya wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Saatano Mahenge na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Ndg. Jordan Rugimbana Oktoba 30, 2017

Imetumwa : October 30th, 2017

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Jordan Rugimbana, Leo Oktoba 30, 2017 amemkabidhi rasmi ofisi Mkuu mpya wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dodoma, Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dodoma, Viongozi wa CCM na Waandishi wa Habari.

Akitoa salamu zake wakati wa kukabidhi ofisi, Ndg. Rugimbana amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa Imani kubwa aliyokuwa nayo kwake tangu alipomteuwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma hadi alipoamua kufanya mabadiliko kwenye safu ya Wakuu wa Mikoa Oktoba 26, 2017 na kuahidi kuwa akiwa uraiani ataendelea kulitumikia Taifa na kuiunga mkono Serikali, lengo likiwa kuhakikisha azma ya Serikali ya awamu ya tano inatimia.

“Pamoja na mabadiliko haya ya Uongozi, daima nitaendelea kukienzi na kukiishi kiapo cha uongozi nilichokula. Aidha, nitaendelea kulitumikia Taifa kwa nguvu zangu zote na kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli” alisisitiza Ndg. Rugimbana.

Pia alishukuru kwa ushirikiano alioupata kutoka kwa taasisi na wadau mbalimbali Mkoani Dodoma wakati wote wa uongozi wake na kuomba ushirikiano huohuo uendelezwe kwa Mkuu mpya wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Mahenge. Pamoja na salamu hizo, Ndg. Rugimbana alimkabidhi Dkt. Mahenge taarifa rasmi ya Makabidhiano yenye Mikakati ya shughuli mbalimbali za maendeleo kwenye Mkoa iliyojumuisha masuala mbalimbali kama Ujio wa Serikali Mkoani Dodoma, Kilimo, Viwanda, Biashara, Uwekezaji na huduma za jamii.

Kwa upande wake Mkuu mpya wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Bilinith Mahenge amesema akiwa Mkoani Dodoma atahakikisha azma ya Rais Magufuli ya Tanzania ya Viwanda inafanikiwa, vilevile atahakikisha anasimamia na kufuatilia shughuli zote za maendeleo kwenye Mkoa, ameomba ushirikiano mkubwa kutoka kwa viongozi mbalimbali Mkoani Dodoma, wadau na wananchi wote ili kuwa timu moja katika kujiletea maendeleo na ametaka kupitia ushirikiano huo kuhakikisha kero na changamoto za wananchi zinamalizwa.

Dkt. Mahenge mara baada ya makabidhiano ya Ofisi, alianza rasmi kazi mara moja kwa kufanya kikao cha kazi na wakuu wote wa wilaya za Mkoa wa Dodoma.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.