• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MAKALA FUPI KUELEKEA MAADHIMIOSHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Imetumwa : March 4th, 2025

Na: Hellen M. Minja,

Habari - DODOMA RS


Maadhimisho ya kilele cha siku ya Wanawake Duniani, hufanyika kila mwaka ifikapo Machi 08. Kuelekea maadhimisho hayo Kitaifa 2025, yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Arusha, huku Mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan,


Mikoa ya Dodoma,Singida na Iringa  imeandaa Kongamano kubwa litakalowakutanisha Wanawake wa mikoa hiyo, Mkoa wa Dodoma ukiwa mwenyeji wa Kongamano hilo  litakalofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma Machi 03, 2025.

Lengo la Kongamano hilo ni  kumtambua Mwanamke katika nafasi ya Uongozi,ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Spika Mstaafu wa Bunge la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Anna Makinda. Ni  hatua muhimu katika mfumo wa maisha ya mwanadamu inayolenga kuhakikisha kuwa na fursa sawa kwa wote na kushiriki kwenye Uongozi na maamuzi yote katika jamii.

Kongamano hilo pia litasadifu lengo la maadhimisho ya siku ya Mwanamke Duniani ambalo ni kuongeza idadi ya Wanawake ili kuwa na uwakilishi wa kutosha kwenye nafasi za uongozi kuanzia ngazi ya msingi,kati hadi juu, kwa wanawake wenye taaluma, utakaosaidia kuwa na mipango inayozingatia mahitaji ya kijinsia kwa makundi yote ya kijamii.

Mpango huu ni pamoja na kupigania kuwepo kwa sera, miongozo, sheria na kanuni ambazo zinalinda haki ya kijinsia na usawa kwenye Uongozi. Wanawake watajengewa ujuzi, taaluma na uwezo wa kujiamini, kujitambua, uthubutu wa kufanya maamuzi na kutenda kwa ajili ya maslahi ya Umma.

Matukio yatakayoambata na Kongamano hilo litakaloanza saa 2:30 asubuhi, ni pamoja na utoaji wa  tuzo/vyeti kwa wananwake vinara waliojitoa na kuwezesha usawa wa kijinsia kwenye jamii, utoaji wa  huduma za afya kwa wananchi watakaoshiriki siku ya kilele, uchangiaji wa  damu, upimaji wa Saratani ya shingo ya kizazi, Saratani ya matiti, upimaji wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza, maonesho ya nishati safi ya mkaa ya vikundi vya wanawake, maonesho ya bidhaa za wanawake wajasiriamali pamoja  na kusikiliza shuhuda mbalimbali kutoka kwa  Wanawake waliofanikiwa wa  Mikoa ya Singida, Iringa na Dodoma.

Siku ya Wanawake Duniani 2025 ambayo Kitaifa hufanyika kila baada ya miaka mitano(5), inakwenda sambamba na kaulimbiu ya “Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji” ambapo matarajio ya Kongamano hilo ni kuwapa mwanga Wanawake ili waweze kujiamini na kupata uzoefu kutoka kwa wanawake vinara kujua mbinu walizopitia hadi kufikia hapo walipo. Wanawake wote wa Dodoma na mikoa jirani wanakaribishwa kushiriki Kongamano hilo.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.