• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA JKT

Imetumwa : July 1st, 2023

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa Jeshi la Kujenga Taifa kuhakikisha wanafanya uwekezaji zaidi katika kufundisha vijana matumizi ya teknolojia katika shughuli zake mbalimbali za uzalishaji mali na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa na Maonesho ya JKT yanayofanyika katika Viwanja vya Suma JKT House eneo la Medeli Mashariki Jijini Dodoma.  Amesema ulimwengu wa sasa ni wakutumia teknolojia na akili zaidi kwa kuwa matumizi ya teknolojia yamedhihirisha uwezo mkubwa wa kuwezesha na kurahisisha utendaji kazi katika nyanja mbalimbali.

Halikadhalika Makamu wa Rais ametoa Rai kwa Jeshi la Kujenga Taifa kuona umuhimu wa kuwatambua wataalam wake wabunifuni na kuwapa tuzo sambamba na kushirikiana na Taasisi husika kuwa na haki miliki ya ubunifu na gunduzi mbalimbali zinazofanywa na Jeshi hilo.

Makamu wa Rais amesema katika kutekeleza dhima ya kuwaandaa vijana wa Tanzania ili kuwajengea nidhamu, uzalendo, ukakamavu na kuwafundisha ujuzi na hatimaye kuchangia katika ulinzi wa Taifa na maendeleo ya kiuchumi, hapana budi kuweka mkazo katika suala la ulinzi na uhifadhi wa mazingira.

Amesema  juhudi za kupanda miti na uhifadhi wa mazingira zifanywe na Kambi zote za JKT nchini, ili kuhakisha mazingira yanatunzwa kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho. Pia amesisitiza  juu ya matumizi ya nishati safi ili kupunguza ukataji miti ovyo pamoja na kutoa msisitizo kwa JKT kuunga mkono udhibiti wa taka za plastiki, kwani huchangia kwa kiasi kikubwa katika uchafuzi wa mazingira.

Aidha Makamu wa Rais ametoa wito kwa Jeshi la Kujenga Taifa kuhakikisha wanashirikiana na Taasisi zingine katika kutafuta suluhisho la upatikanaji wa chakula cha samaki hapa nchini. Pia amesisitiza taasisi za kifedha ikiwemo Mabenki kutoa elimu kwa Vijana wa JKT na kuwawezesha upatikanaji wa mikopo ili waweze kujiajiri pindi wanapohitimu mafunzo yao.

Vilevile Makamu wa Rais ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika wiki nzima ya maadhimisho ya miaka 60 ya JKT ili kuweza kujionea bidhaa mbalimbali zinazozalishwa pamoja na kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo kilimo, ufugaji na utengenezaji bidhaa.

Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Innocent Bashungwa amesema Wizara itaendelea kuijengea JKT uwezo ili kuweza kuongeza uzalishaji wake kupitia Suma JKT na kushiriki katika miradi mikubwa ya kimkakati. Amesema kwa kushirikiana na Wizara zingine za kisekta wanatarajia kuboresha mafunzo ya stadi za kazi kwa vijana wa JKT na kuwawezesha kuwapatia ujuzi na maarifa zaidi ili baada ya kuhitimu waweze kujitegemea kwa kuanzisha shughuli mbalimbali za ujasiriamali.

Waziri Bashungwa ameongeza kwamba pamoja na malezi kwa vijana JKT inapaswa kuwa na ubunifu na kutoa mchango kwa taifa, kuzalisha ajira na kulisaidia taifa kuwa na chakula toshelevu.

Awali akitoa taarifa juu ya Maendeleo ya Jeshi la Kujenga Taifa, Mkuu wa Jeshi hilo Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema licha ya changamoto mbalimbali JKT imefanikiwa kufikia dhumuni la kuanzishwa kwake kwa kutoa mafunzo ya malezi kwa vijana ili kuwajengea uzalendo, kujitegemea na kuleta maendeleo endelevu na utangamano wa kitaifa. Amesema malengo hayo yametekelezwa kwa ufanisi na kufanikiwa kuwabadili vijana kifikra, kuwajenga katika hali ya umoja, moyo wa kupenda kazi, uadilifu, nidhamu, uzalendo na uelewano bila kubaguana kwa misingi ya ukabila, udini, jinsia na kudumisha uhuru na amani ya Taifa.

Meja Jenerali Mabele ameishukuru serikali kwa kuendelea kuchukua hatua mbalimbali kukabiliana na changamoto za Jeshi hilo ikiwemo kuendelea kutenga fedha ili kuboresha miundombinu itakayowezesha kuchukua vijana wengi zaidi kwaajili ya mafunzo.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.