• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MAONESHO YA KITAIFA YA NANENANE SASA YATAFANYIKA KWENYE KITUO KIMOJA CHA KUDUMU KWA MIAKA YOTE BILA KUHAMAHAMA KAMA ILIVYOSASA

Imetumwa : August 5th, 2017

Serikali inafikiria kuwa na kituo kimoja cha Kitaifa cha kufanyia Maonesho ya Kitaifa na Kimataifa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Nane Nane) na kuachana na utaratibu wa kuhamishahamisha Maonesho hayo kama ilivyo sasa yanafanyika kwenye Kanda tofautitofauti, akitolea mfano mzuri Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba ambayo yanafanyika sehemu moja tu ya Dar es salaam na huku Mikoani yanafanyika kwa ngazi za Mikoa.

Ameongeza kuwa Serikali pia inafikiria kuanzisha chombo cha Kitaifa cha kusimamia Maonesho haya ya Nane Nane kwa miaka yote kama ilivyo kwa taasisi ya TANTRADE ambayo inasimamia Maonesho ya Sabasaba akiutaja utaratibu huu kuwa utawezesha Maonesho ya Nane Nane kupaa Kitaifa na Kimataifa.

Mheshimiwa Dkt. Tizeba ameyasema hayo Agosti 5, 2017 wakati wa kilele cha Paredi ya Mashindano Maalumu ya saba (7) ya Mifugo ya Kitaifa yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kati vilivyopo Nzuguni nje kidogo ya Mji wa Dodoma.

Amesema Utaratibu wa kuhamahama Kanda kwenye kufanya Maonesho ya Nane Nane unasababisha wadau wenye nia ya kutaka kushiriki kwa kuwekeza miundombinu ya kudumu ya gharama kubwa kushindwa kufanya hivyo kwa kuhofia kupoteza rasilimali zao sehemu moja na kisha mwaka mwingine Maonesho yanahama. Hiyo pia inachangia Maonesho yetu kukosa umaarufu Kitaifa na hata Kimataifa.

Amewataka wadau wote wanaosimamia na kuendesha Nane Nane kuchukua mfano mzuri wa Maonesho ya Sabasaba Kitaifa ambayo hayahami, yako Dar es salaam miaka mingi. Mheshimiwa Tizeba amesema tukiweza kuwa na kituo kimoja cha Maonesho, tutawezesha hata wale wenye kutaka kuwekeza miundombinu ya kudumu na gharama kubwa kuweza kufanya hivyo bila kuwa na hofu ya kuhama kwa Maonesho, pia kutapunguza migogoro ya Kisiasa ambayo ilisababishwa na wanasiasa waliokuwa wakigombania Maonesho ya Nane Nane kupelekwa kwenye Kanda zao.

Katika hatua nyingine Mheshimiwa Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Charles Tizeba amewaonya vikali wananchi wenye tabia ya kuuza chakula chote walichovuna na kisha kukabiliwa na njaa kwa uhaba wa chakula na kuanza kusumbua Wakuu wa Wilaya na Mikoa wakitaka Serikali iwape chakula ili kukabili njaa inayowakabili badala yake amewataka wananchi waliovuna chakula watunze chakula hiko hadi watakapokutana na mavuno ya msimu ujao.

“Wako watu ambao wamefanya kama utaratibu, wanavuna wanauza chakula chote halafu wanaliamsha kuwa wanakabiliwa na njaa ili baadhi ya watu tukose usingizi kwa kuwa wananchi wanakabiliwa na njaa, safari hii ukiuza hata ukiliamsha vipi halitaamka” alionya Mheshimiwa Tizeba.

Amesema tathimini ya awali iliyofanywa na Serikali imebaini mavuno ya msimu wa mwaka huu wa kilimo yanatosheleza mahitaji ya chakula kwa asilimia 120 kiwango ambacho kimeshuka kulinganisha na asilimia 123 ya mwaka jana. Hata hivyo, Dkt. Tizeba amesema kiwango hiko kinatosheleza mahitaji ya chakula tuliyonayo endapo kitatumika kwa uangalifu.

Nae Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Nane Nane Kanda ya Kati Bi. Aziza Mumba alibainisha kuwa mwaka huu 2017 yanafanyika Maonesho ya kumi (10) katika uwanja wa Nzuguni. Kwa upande wa mifugo yanafanyika Maonesho ya saba (7) Kitaifa kuanzia mwaka 2011. Uwanja wa Nzuguni ni kituo cha kudumu kwa Maonesho ya mifugo Kitaifa. Amesema kwa miaka yote 8 ya nyuma, kulikuwa na mahudhurio makubwa ya watazamaji na waoneshaji.

Ametaja Kaulimbiu ya mwaka huu 2017 ni “ZALISHA KWA TIJA MAZAO NA BIDHAA ZA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI ILI KUFIKIA UCHUI WA KATI” akihusisha na Malengo ya Maonesho ya Mwaka huu kuwa ni utoaji wa elimu ya matumizi ya teknolojia mbalimbali kwa wadau wengi kwa muda mfupi. Wadau watajifunza kwa njia ya kuona, kujadiliana na kuulizana maswali. Maeneo makuu ya mafunzo ni teknolojia za uzalishaji wenye tija wa mazao, mifugo na usindikaji wa bidhaa kuongeza thamani. Teknolojia nyingine zitakazooneshwa ni hifadhi ya mazingira, vyanzo vya nishati mbadala, zana na pembejeo bora za kilimo na mifugo zipatikanazo nchini na teknolojia za mawasiliano.

Ameongeza kuwa Wadau pia watajionea na kujifunza huduma zitolewazo na Serikali, Mashirika ya umma na binafsi, Aidha Maonesho hutumiwa na wafanyabiashara kuuza bidhaa, kufahamiana na kuingia makubaliano. Halikadhalika, watu wamekuwa wakipata fursa ya kuwaona baadhi ya wanyamapori katika Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.