• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MASOMO YA AMALI YATAWAWEZESHA VIJANA KUTOKA NA UJUZI-RC SENYAMULE

Imetumwa : March 25th, 2025

Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS


Serikali ya awamu ya sita imeingiza Mtaala mpya wa elimu unaohusisha masomo ya ufundi (Amali) ili kuwawezesha vijana wanaomaliza kiwango fulani cha elimu kutoka na ujuzi ambao utawawezesha kujiajiri wenyewe pasi na kutegemea kuajiriwa.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, ameyasema hayo alipokua kwenye hafla ya uzinduzi wa bweni na jengo la michezo kwenye shule ya Wavulana ya ‘The Sisters of Mary Boystown’ iliyopo eneo la Kikombo, Jijini Dodoma Machi 25, 2025 ambayo inafundisha masomo ya kawaida na  Amali upande wa TEHAMA.


“Hapa mnakwenda sambamba na dhamira ya Serikali ya kutilia mkazo masuala ya ufundi. Wote mnajua kuwa Serikali hivi karibuni ilizindua Sera mpya ya elimu pamoja na mtaala ambapo masomo ya ufundi yameingizwa kwa lengo la kuwawezesha vijana kiwango fulani cha elimu waweze kutoka na ujuzi” Mhe. Senyamule


Kadhalika, akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Elimu Prof. Adolf Mkenda, Kamishna kutoka Wizara hiyo Bw. Abdul Maulid amesema Wizara yake imefanya maboresho ambayo tayari yameshafanywa na shule hiyo ambayo ni uwepo wa mikondo miwili, ya kawaida na ile ya Amali hivyo amewaasa wanafunzi hao kuleta maendeleo kwa jamii kutokana na elimu wanayoipata shuleni hapo.


Askofu Mkuu Jimbo Katoliki Mkoa wa Dodoma Beatus Kinyaiya, amewaasa wanafunzi hao kuzingatia mafunzo ya Amali wanayoyapata shuleni hapo huku akiishauri Serikali kutafuta namna bora itakayofanya mtaala huo mpya kutengeneza vijana wabunifu na si kujaza wataalamu ambao hawatakua na tija kwenye jamii.


Aidha, Kiongozi wa Masista katika shule hiyo Bi. Elena G. Belarmino amesema kwa msaada wa Askofu Kinyaiya, walipata eneo hilo na kujenga shule mwaka 2022 ambapo sasa ni Mji wa Wavulana wanaofikia 370 kutoka katika familia duni Nchi nzima wanaopata elimu shuleni hapo.


Shule ya ‘The Sisters of Mary Boystown’ imeasisiwa na Bw. Aloysius Schwartz, raia wa Korea ambapo inasimamiwa na Masista kutoka Nchini humo na Ufilipino na kwa sasa inatoa elimu bure kwa wavulana hao kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita kwa kupata msaada kutoka kwa wafadhili wa nchi mbalimbali zikiwemo Ujerumani na Marekani.




#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.