• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MGAMBO WAONYWA KUNYANYASA WAFANYABIASHARA WADOGO

Imetumwa : March 1st, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, ametoa onyo kwa mgambo wa Jiji wanaowanyasa wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga kwa kuwamwagia bidhaa zao kwani hayo sio maagizo ya Serikali na kufanya hivyo ni kukiuka haki za wafanyabiashara hao. Hayo yamesemwa wakati wa uzinduzi wa kituo cha daladala kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria kwenye soko kuu la machinga complex lililopo eneo la Bahi Road Jijini Dodoma.

Kituo hiki kinachopokea daladala kutoka pande zote za Jiji la Dodoma, kimezinduliwa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alilotoa wakati alipowatembelea wafanyabiashara hao na kuzungumza nao hivyo walipata fursa ya kufikisha ombi hilo na huu ni utekelezaji wake.

“Kinachofanyika hapa ni utekelezaji wa maagizo ya Serikali. Sitoi kibali kwa mgambo kutumia nguvu kwa wafanya biashara kwani haya sio maelekezo ya Serikali. Tusipige watu wala kunyang’anya bidhaa zao ingawa bado sheria zetu zinatutaka tusifanye biashara kwenye maeneo yasiyoruhusiwa. Lililotuleta hapa ni uzinduzi wa Kituo cha Daladala, tunakwenda kushuhudia daladala zote zikianzia hapa. LATRA na Polisi endeleeni kushirikiana kupanga kila daladala inayopaswa kuingia hapa” Amesema Mhe. Senyamule

Kadhalika, Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma Prof. Davis Mwamfupe ametoa pongezi kwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwani Dodoma imepata fursa ya kutafsiri maono yake kupitia uzinduzi wa kituo hiki.

“Dodoma tumepata fursa ya kutafsiri maono ya Mhe. Rais kwa tukio hili. Namshukuru kwa kuona umuhimu wa Serikali kuwatambua wafanyabiashara hawa. Ninyi ni kiungo maalumu katika kuhudumia wananchi wa Dodoma, viongozi wa daladala wametupa ishara kwamba wanajitambua nah ii ndio Dodoma tunayoitaka, yenye utaratibu” Amepongeza Dkt. Mwamfupe

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Bw. Joseph Mafuru, amesema kuwa wameyatekeleza maagizo yote yaliyotolewa na Waziri Mkuu ikiwemo hili la kuweka kituo cha daladala katika soko na kuweka taa za barabarani katika eneo hili kwani hapa wafanyabiashara wanafanya shughuli zao mpaka majira ya usiku pia kwa sasa wanatekeleza agizo kuwapatia mikopo wafanyabiashara hao.

Pia Afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti na Usafirishaji wa Nchi kavu Tanzania (LATRA) Bw. Ezekiel Emmanuel, amesema kuwa wameanza kuhamisha daladala zote kutoka kituo cha sabasaba kwa kushirikiana na wadau wote wanaohusika na usafirishaji  na takribani daladala 850 zinatarajiwa kutoa huduma kwenye kituo hiki kipya na wao kama mamlaka husika wanasimamia uratibu huo. Ameongeza kuwa LATRA wanaendelea kushirikiana na Halmashauri ya Jiji kuboresha huduma hii kwa kutoa matangazo kwa njia ya magari kupita mitaani yakiwa na vipaza sauti kuwaelekeza wananchi juu ya matumizi sahihi ya njia hizi zinazoingia na kutoka sokoni hapo.

                                                                                    

MWISHO

 

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.