• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MHE. JAFO: UWANJA WA NANE NANE NZUGUNI MKOANI DODOMA UNAFAA KUWA KITUO CHA KUDUMU CHA MAONESHO YA KITAIFA YA WAKULIMA, WAFUGAJI NA UVUVI

Imetumwa : August 8th, 2017

Siku mbili baada ya Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Dkt. Charles Tizeba kusema kuwa Serikali inafikiria kuachana na utaratibu wa kuhamishahamisha Maonesho ya Nane Nane kwenye Kanda mbalimbali na badala yake kuwa na kituo kimoja cha Kitaifa cha kufanyia Maonesho hayo ya Kitaifa na Kimataifa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Nane Nane) kama ilivyo kwa maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanavyofanyika Dar es Salaam pekee, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Suleiman Jafo ametoa Wito kwa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kuamua kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa Kituo cha Kudumu cha Maonesho hayo.

Amesema kuwa Dodoma ni Makao Makuu ya Nchi hivyo kuifanya kuwa kituo cha kudumu cha Maonesho hayo ya Nane Nane ni kuunga Mkono uamuzi wa Mheshimiwa Rais Magufuli wa kuihamishia Serikali Mkoani Dodoma.

“Kijiografia pia Mkoa wa Dodoma ambao ndio Makao Makuu ya nchi upo katikati ya Nchi na hivyo ni rahisi kwa Kanda zote nchini na hata nchi za jirani kuja kushiriki Maonesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni” ameongeza Mheshimiwa Jafo.

Mheshimiwa Jafo ameyasema hayo Agosti 8, 2017 wakati wa hafla ya kugawa zawadi kwa washindi wa Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kati yaliyoanza tangu Agosti Mosi ambapo Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limeibuka kuwa Mshindi wa jumla wa Maonesho ya Mwaka huu, likifuatiwa na Benki Kuu ya Tanzania ikiwa mshindi wa pili na Mshindi wa tatu likiwa Jeshi la Magereza.

Amesema kuwa Uwanja wa Nane Nane Nzuguni unahitaji kufanyiwa uwekezaji na uendelezaji wa miundombinu yake kama barabara, umeme na maji na kuboreshwa huduma mbalimbali na kuzitaka Mamlaka za Serikali za Mikoa ya Dodoma na Singida kuweka mkakati wa kuendeleza miundombinu hiyo na hata ikibidi kushirikisha Taasisi kama Benki ya Uwekezaji TIB na Benki ya Maendeleo ya Kilimo TADB kwa kuwa baada ya uwekezaji mkubwa uwanja huo utarejesha mapato mengi.

Akizungumzia Kaulimbiu ya Maonesho ya Nane Nane Mwaka huu inayosema “Zalisha kwa Tija Mazao na Bidhaa za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati” amesema kuwa kwenye Maonesho amejionea taaluma na Elimu kubwa za namna Wakulima na Wafugaji wetu watumie pembejeo, zana bora na teknolojia pia kuongeza tija katika shughuli zao za Uzalishaji wakati jukumu la Halmashauri za Wilaya ni kupeleka mambo hayo yote kwa Wakulima ngazi za Msingi.


Ili kuhakikisha mazao ya kilimo na mifugo yanapata soko na yanachakatwa na kufungashwa kwa lengo la kuyaongezea thamani, amezitaka Halmashauri za Wilaya kutenga Maeneo maalumu kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda na kuhakikisha maeneo hayo yanakuwa na huduma zote za msingi kama vile miundombinu ya Barabara, Umeme na Maji amesema Jafo na kuongeza kuwa tukifanya hivyo tutamuwezesha Mkulima na Mfugaji kufikia uchumi wa kati.


Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Ole Nasha ameipongeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo kwa kuendelea kuwezesha shughuli za kilimo lakini amewapa angalizo la kuto kuegemea kuwawezesha mikopo kwa watu wenye uwezo tu na kusahau jukumu lao la kuwafikia hata wakulima wasio na uwezo na kuwapatia mikopo waweze kufanya kilimo cha kisasa na kujikwamua kimaisha.

Kwa upande wake Mheshimiwa Simon Odunga Mkuu wa Wilaya ya Chemba Dodoma kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa ya Dodoma na Singida ambao ndio Wenyeviti wa Kamati ya Nane Nane Kanda ya Kati ameweka msisitizo wa maamuzi ya Serikali za Mikoa hiyo miwili ya kuongeza siku mbili (2) zaidi za kuendelea kufanyika Maonesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni hadi Agosti 10, 2017.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.