• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MHE. SENYAMULE AKUTANA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA

Imetumwa : January 5th, 2023

MKUU WA MKOA WA DODOMA AONGEA NA VYAMA VYA SIASA

Viongozi wa Vyama vya Siasa Mkoa wa Dodoma wametakiwa kufanya siasa na kuendesha mikutano ya vyama vyao kwa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, ameyasema hayo Januari 5, 2023 wakati wa kikao baina yake na viongozi wa vyama vya siasa wa Mkoa wa Dodoma katika ukumbi wa ofisi yake jengo la Mkapa.

Amesema lengo la kukutana na vyama hivyo ni kukakikisha wanajipanga kutekeleza kwa ufanisi maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokutana na viongozi wa Siasa Taifa Jijini Dar es Salaam Januari 03 mwaka huu, ili Mkoa wa Dodoma na Vyama vya siasa waweze kuratibu utekelezaji wa maelekezo hayo kwa kushirikiana

Akifungua kikao kicho Mhe. Senyamule amesema ni vema Mkoa na vyama hivyo kukutana na kupanga namna watakavyofanikisha utekelezaji na uratibu wa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa kwa amani na kudumisha usalama wa Mkoa ambapo Mhe. Senyamule alitoa nafasi kwa viongozi na waliwakilisha wa vyama takribani 14 vilivyopo hapa Dodoma kutoa maoni yao juu ya mustakabali huo.

Viongozi wa vyama vya siasa waliopata fursa ya kuzungumza ni pamoja na CCM, CHADEMA, CUF, Demokrasia Makini, Sauti ya Umma, NCCR – Mageuzi na TLP kwa pamoja wamempongeza Mhe Dkt. Samia suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwaruhusu kufanya mikutano ya hadhara ya kisiasa toka kusitishwa kwake takriban miaka saba sasa.

Wameiomba Serikali ya Mkoa kutoa ushirikiano wa kutosha pale wanapohitaji kufanya mikutano yao ikiwemo kuhitaji ulinzi na usalama wa jeshi la polisi na kusisitiza utawala wa Demokrasia.

Mhe. Senyamule amesema kuwa  Serikali ya Mkoa itatekeleza maagizo ya Mhe. Rais kama alivyoelekeza;

“Tumekua tukiiga mazuri yanayofanywa na Rais wetu ikiwemo hili hivyo twende tukayatekeleze. Rais ameweka historia ya miaka saba tangu kuzuiwa kwa mikutano ya hadhara na amekua na matamanio ya kutuona wote tukiwa wamoja. Tutatekeleza maagizo na maelekezo ya Amiri Jeshi Mkuu kama alivyoelekeza, twende tukayatekeleze.” Amesema Mhe. Senyamule

Halikadhalika, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. Martin Otieno amewahakikishia viongozi hao wa vyama vya siasa ulinzi na usalama wao wakati wote wa mikutano yao muhimu ni kufuata sheria za kuendesha mikutano ya hadhara.

“Jeshi la Polisi litatoa ushirikiano kwa vyama vyote vya Mkoa, muhimu ni kufuata sheria kwani ipo na imeainisha taratibu na miongozo ya kufanya mikutano ya vyama vya siasa. Tutahakikisha mikutano yote itakayoombewa vibali, inapewa ulinzi na usalama” Amesema Kamanda Otieno

Vilevile M-NEC wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Bw. Donald Mujeti amesema kuwa Chama chake ambacho ndicho chama tawala kinaahidi kutoa ushirikiano kwa vyama vingine kwa kufanya siasa za kistaarabu kwani wao ni kioo cha siasa nchini na kusisitiza kuwa watakua mfano wa kuigwa kwa kufanya siasa za kistaarabu na bila kuharibu hali ya usalama”

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.