• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MHE. SENYAMULE AONGOZA ZOEZI LA UPANDAJI MITI CHEMBA

Imetumwa : January 4th, 2023

ELIMU YA KUJITEGEMEA ITOLEWE SHULENI

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema Kampeni ya “Soma na Mti” iendelee kusisitizwa shuleni, Watoto wafundishwe kutunza mazingira kwa kupanda miti na kusimamia miradi itakayowafundisha watoto elimu ya kujitegemea kama kilimo

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alipokua akiongea na wanachi kwenye muendelezo wa kampeni aliyoizindua ya upandaji miti kwa  Mkoa wa Dodoma ambapo alipanda miti katika eneo la Hospitali ya Wilaya ya Chemba.

Mkuu wa Mkoa amewasihi wakazi wa Chemba kutunza uoto wa asili uliopotea ili kutunza uumbaji wa Mungu kwa kupanda miti ikiwa ni utekelezaji pia wa Kampeni ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani kwa kuhakisha kila Halmashauri inapanda miti 1,500,000 kwa mwaka.

“Maelekezo ya viongozi wa juu ni kila Halmashauri kupanda miti 1,500,000 kila mwaka hivyo nina imani kila Halmashauri imejipanga kwa kuandaa miche ya kutosha. Hapa leo tunapanda miti 300, tunataka tukirudi mwakani tuikute hii miti 300” Amesisitiza Mhe. Senyamule

Kadhalika, Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe. Simon Chacha amesema kuwa Wilaya yake bado ina  miti mingi ya asili na wakazi wa hapo ni watunzaji wazuri wa miti. Ameongeza kuwa Wilaya imejipanga kupanda miti 10,000 kwa kipindi hiki cha msimu wa mvua na zoezi hilo litafanyika kwenye taasisi zote za Serikali na lengo ni kuhakikisha miti iliyopandwa inastawi.

Mbali na kuhamasisha kampeni ya kupanda miti. Mhe. Senyamule pia ametembelea baadhi ya shule za Wilaya hiyo kuangalia maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023 wanaotarajiwa kuanza muhula mpya wa masomo yao tarehe 09 Januari.

Miongoni mwa shule alizotembelea ni shule za sekondari Goima, Songoro, Mrijo na Soya ambazo zote zinaendelea na ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa.

“Tujifunze namna ya kusimamia miradi hii kwani bado kuna miradi mingi inakuja. Hakikisheni miradi inakamilika kwa wakati, tuanze kujipanga sasa kwa miradi ijayo kwa kutumia uzoefu wa miradi hii” Mhe. Senyamule

Mkuu wa Mkoa amewataka watendaji wa vijiji kufuatilia wazazi nyumba hadi nyumba kuhakikisha wazazi wanapeleka Watoto shuleni kwani madarasa yapo ya kutosha kwa kuwa Mkoa umedhamiria kupambana na utoro shuleni.

“Tumedhamiria kutokomeza utoro shuleni hivyo wazazi hakikisheni shule kila mtoto anakwenda shule msimu huu kwani sheria zipo na zinatutaka kuchukua hatua kwa mzazi asiyepeleka mtoto shule” Ameongeza Mhe. Senyamule

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.