• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MIRADI YOTE IKAMILIKE KWA WAKATI - GUGU

Imetumwa : April 13th, 2023

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu amesema lengo na matarijio  ya Mkoa nikuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa kuzingatia muda uliowekwa na viwango vya ubora unaotakiwa kwa kuzingatia thamani ya fedha.

Gugu  ameyasema hayo leo tarehe 13/04/2023 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika Wilaya ya Bahi kwa lengo la kukagua utekezaji wa miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo.

Gugu amehimiza watumishi wanaosimamia miradi hiyo kuwajibika na kuhakikisha usimamizi madhubuti wa miradi yote ya maendeleo na kutoa angalizo juu ya hatua zitakazochukuliwa dhidi ya miradi ambayo haitakamika kwa wakati na ubora unaotakiwa.

“Serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeleta fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya afya na elimu katika Halmashauri zetu, tusiwe moja ya vikwazo katika kusimamia ukamilifu wa miradi hii, tunatoyaka kufanya yafanyike kwa wakati na hapa nisisitize kubwa zaidi kusiwe na viporo vya kutokamilika kwa miradi ya maendeleo. Sote tudhamirie  kukamilisha kazi zote zilizopangwa kutekelezwa katika mwaka huu wa fedha kwa kuzingatia mpango kazi” Gugu alisisitiza.

Awali, Katibu Tawala Bw. Gugu alipata wasaa wa kuzungumza na Watumishi wa Wilaya ya Bahi na kuwataka kutumiza wajibu wao kwa kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni za Utumishi wa Umma.

“Haki zinaenda sambamba na wajibu, hivyo timizeni wajibu wenu kikamilifu kila mmoja katika nafasi yake”

Halmashauri ya Wilaya ya Bahi iko katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa majengo 18 kati ya majengo 28 yanayotakiwa kwenye hospitali ya Wilaya ambapo  jumla ya Shilingi Bilioni 4.3 zimetumika.

Kutokana na kukamilika kwa baadhi ya majengo katika Hospitali hiyo imewezesha kuanzishwa kwa huduma ya mionzi, huduma ya upasuaji ambapo mpaka sasa akina mama 212 wamefanyiwa upasuaji, uwepo wa huduma za X-Ray na Ultrasound na kutoa huduma kwa watoto waliozaliwa chini ya umri kamili wa mimba yaani Watoto njiti.

Bw. Gugu katika ziara yake amekagua pia ujenzi wa Zahanati ya Nagulo, Shule ya Msingi Bahi English Medium Pre and Primary School, Shule ya Msingi Mpamantwa Barabarani na Shule ya Msingi Kigwe yenye wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.