• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MITUNGI YA GESI 1000 YAGAWIWA KWA MAKUNDI MAALUM JIJINI DODOMA

Imetumwa : September 20th, 2024

Katika harakati za kuunga mkono jitihada za Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule amegawa mitungi 1000 ya gesi ya kupikia kwa makundi mbalimbali ya jijini humo. 

 Hafla ya ugawaji wa mitungi hiyo imefanyika leo Septemba 20, 2024 kwenye viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza utunzaji wa mazingira sanjari na kuboresha afya husuani za kina mama wanaotumia nishati hiyo kupikia.

 “Mkakati umetengenezwa Katika kipindi cha miaka kumi kuanzia 2024 hadi 2034 ambao utatuongoza watanzania namna ambavyo 80% ya watanzania kufikia 2034 wawe tayari wanatumia nishati safi, kwa kuanza na makundi yenye watu wengi, taasisi zenye mikusanyiko mikubwa na zinazotumia nishati chafu kwa wingi” Amesema Mhe. Senyamule 

Hata  hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mh. Jabir Shekimweri, ametoa tathmini ya athari ya matumizi ya nishati chafu kwa afya.

 “Takwimu zinaonesha watu Milioni 4 hufariki mapema duniani kutokana na kutumia nishati chafu. Wakati wa uzinduzi wa mkakati huu kitaifa, takwimu zilitolewa, watu 33,000 hufariki kila mwaka nchini kwa matumizi ya nishati chafu hususan mkaa. Ukitafsiri takwimu hizo, watu 33,000 ni wastani wa watu 2850 kwa mwezi na 88 kila siku” Amesema Mhe. Shekimweri 

Aidha, Waziri wa Madini na Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde ambaye ndiye mfadhili wa mitungi hiyo, ametaja lengo kuu la kutoa mitungi hiyo kwa makundi ya jimbo lake. 

 “Kwa kushirikiana na Jiji la Dodoma, tutaendelea kuhakikisha matumizi ya teknolojia mbadala ya matumizi ya mkaa mbadala ambao hauna madhara kwa mazingira, mkaa wa kutumia makaratasi, plastiki na magome ya ndizi ili tuweze kuwasaidia watu wetu kuachana na zoezi la kukata miti ili kupunguza uharibifu wa mazingira, dunia iwe sehemu salama ya kuishi” Mhe. Mavunde 

Hafla ya ugawaji wa mitungi na majiko ya gesi, imefanywa na Mbunge huyo ikiwa ni endelevu ambapo sasa inatimiza jumla ya mitungi 2500 iliyogawiwa tangu kuanza kwa zoezi hilo. Mitungi na majiko hayo imegawiwa kwa shule, Zahanati, Vituo vya afya, vituo vya watoto yatima na mama na baba lishe.    

                                                                         #keroyakowajibuwangu #dodomafahariyawatanzania












ReplyForward


Add reaction










Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.