• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MKUU WA MKOA NA WAKUU WA WILAYA WASAINI MIKATABA YA LISHE

Imetumwa : October 19th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule,  hivi karibuni amesaini mkataba wa utendaji kazi za lishe baina yake na wakuu wa Wilaya ambao unaratibiwa na kusimamiwa na idara ya afya Mkoa. Shughuli hiyo imefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Lengo kubwa la mkataba huu ni kufanikisha suala la kuboresha hali ya lishe na kupunguza athari za utapiamlo katika Halmasahauri, kuhakikisha Halmashauri inasimamia ipasavyo utekelezaji wa afua za lishe pamoja na  kuchukua hatua madhubuti za kupunguza hali duni ya lishe katika halmashauri.

Akiongea, mara baada ya kusaini mkataba huo , Mhe.Senyamule amesema kuwa mkataba huo umepewa uzito wa pekee na Serikali ndio maana wamesaini na amewataka wakuu wa Wilaya kwenda kuutekeleza. “Twende tukaupe uzito mkataba huu na tukautekeleze, tuongeze ufanisi na ubora kwenye hili kwani Dodoma bado tuna tatizo la lishe kwani tunaambiwa udumavu upo kwa asilimia 37 hivyo tuna kazi kubwa ya kufanya kwa ajili ya lishe”

Hata hivyo, Mhe. Senyamule ametoa maelekezo juu ya upandaji miti ya matunda kwani matunda yanasaidia katika kuboresha lishe hasa kwa Watoto.

“Tufanye vikao na tathmini za uhalisia juu ya tatizo la lishe na mukasimamie zoezi la upandaji miti ya matunda ili watoto wapate matunda kwa afya” Amesisitiza Mhe.Senyamule.

Utekelezaji wa mkataba wa utendaji kazi za lishe unasimamia pia utoaji wa taarifa kwani kila Wilaya itatakiwa kuwasilisha taarifa za utendaji kazi za kila robo mwaka kila ifikapo tarehe 07 ya mwezi unaofuata huku taarifa ya utendaji kazi ya mwaka ikitakiwa kuwasilishwa kabla ya tarehe 16 ya mwezi Julai ya kila mwaka.

Aidha, mkataba huu wa kiutendaji utakua wa muda wa miaka nane (8) na umeanza rasmi Julai Mosi, 2022 hadi Juni 30, mwaka 2030 na utakua ukipimwa kila mwisho wa mwaka husika. Iwapo utajitokeza mgogoro wowote katika utekelezaji wake, pande zote mbili zitakaa pamoja ili kutatua mgogoro huo.

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.