• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge Amekutana na Kufanya Mazungumzo na Viongozi wa Madhehebu ya Dini Mkoani Dodoma na Kuahidiana Kuendeleza Ushirikiano, Novemba 8, 2017

Imetumwa : November 8th, 2017

MKUU WA MKOA WA DODOMA DKT. BINILITH MAHENGE AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA MADHEHEBU YA DINI MKOANI DODOMA NA KUAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO, NOVEMBA 8, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge ameendelea na ratiba ya kukutana na Kuzungumza na Viongozi wa makundi mbalimbali muhimu kwenye Mkoa wa Dodoma na awamu hii amekutana na Viongozi wa Madhehebu ya Dini na wajumbe wa Kamati ya Amani na Mahusiano kwa lengo la kuendelea kujitambulisha na kushauriana namna ya kuendeleza ushirikiano mzuri uliopo baina ya Serikali na viongozi wa Madhehebu ya Dini.

Dkt. Mahenge amesema Serikali inatambua mchango mkubwa wa Viongozi wa Dini hususani kwenye eneo la ulinzi wa Amani kiroho lakini pia kwenye upande wa ushiriki wa miradi mbalimbali ya huduma za jamii kama Afya, Elimu na nyingine nyingi na hivyo kuwataka waendelee kutoa ushirikiano kwa Serikali ili kuhakikisha Mkoa wa Dodoma unapiga hatua muhimu za Maendeleo.

Amewataka viongozi hao wa Madhehebu ya Dini kushirikiana na Serikali kwenye masuala Makubwa ya Kitaifa kama ujio wa Serikali Mkoani Dodoma na masuala mengine ya Maendeleo kama kusaidia kwenye sekta ya Elimu kuhamasisha ukuaji wa kiwango cha Elimu na ufaulu kwenye Mkoa, Kilimo hususani kuhamasisha juu ya uzalishaji wa chakula chenye kutosheleza mahitaji na kwa ajili ya biashara.

Sheikh wa Mkoa wa Dodoma na Qadhi Mküu wa Mkoa Dodoma ambaye pia ndio Mwenyekiti wa kamati ya Amani na Mahusiano ya Viongozi wa Dini Sheikh Mustwafa Rajabu Shaaban amemhakikishia Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Mahenge kuwa, viongozi wa Dini Mkoani Dodoma wanaiunga Mkono Serikali na kuwa wanamuhakikishia ushirikiano kwenye majukumu yake, lakini pia wataendelea kushiriki kwenye majukumu ya kuiasa jamii juu ya Amani pia kushiriki kwenye shughuli za Maendeleo ya Mkoa wa Dodoma hususani eneo la huduma za jamii.

Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Amani na Mahusiano ya Viongozi wa Madhehebu ya Dini ambaye pia ni Askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Dodoma Askofu Amon Kinyunyu amesema wanaiunga Mkono Serikali kwenye kuhamia Makao Makuu ya Nchi Dodoma na kusema kuwa tayari baadhi ya Taasisi zao za Dini tayari zimeanza mchakato wa kuandaa Makao Makuu ya Taasisi zao kwenye Mkoa wa Dodoma.

Ameomba Mkuu wa Mkoa kuhakikisha kuwa anazisimamia kwa umakini mkubwa Taasisi mbalimbali za Serikali Mkoani Dodoma zenye kutoa huduma zinazohusiana na ujio wa Serikali ili ziendane na kasi ya ukuaji wa Makao Makuu, wakizitaja Taasisi hizo kama vile zinazosimamia huduma za Maji (DUWASA), Mamlaka za Ardhi ambazo mara nyingi zimeshutumiwa kusababisha migogoro mingi ya Ardhi na bughudha kwa wananchi.

Viongozi hao wa Madhehebu ya Dini wamewasilisha ombi maalumu kwa Mkuu wa Mkoa kuzisaidia Taasisi za Madhehebu ya Dini kupata maeneo ya Ardhi ya Kutosha kwenye mji wa Dodoma kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Taasisi zao, Ombi ambalo Dk. Mahenge ameahidi kama ambavyo serikali inatenga Eneo la Ardhi kwa ajili ya Ujenzi wa Balozi mbalimbali hapa nchini, basi ataziagiza Mamlaka za Ardhi Mkoani Dodoma kutenga Maeneo Maalumu ya Ardhi kwa ajili ya Taasisi za Dini.

Viongozi hao wa Madhehebu ya Dini Wameomba Mkuu wa Mkoa Dkt. Mahenge kufikisha Salamu zao za shukrani na pongezi kwa mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuhamishia Serikali yake Mkoani Dodoma kwa kusema kuwa uamuzi huo unairudishia Mkoa wa Dodoma heshima yake uliyopewa miaka mingi iliyopita.

Kiongozi wa Taasisi ya Kiislamu ya Dalai Islamic ya Mjini Dodoma Alhaji Rashid Bura amempongeza Mheshimiwa Rais Magufuli kwa jitihada zake za uongozi, Udhibiti wa Rasilimali za Taifa kama madini kwa manufaa ya Watanzania wote, Uboreshaji wa Utumishi wa Umma na kurudisha nidhamu, kusimamia ukusanyaji mapato na udhibiti wa matumizi ya Serikali, Utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kubwa Zaidi Serikali yake kuwa serikali yenye kuwajali zaidi Watanzania Masikini na Wanyonge na kuhakikisha wanapata huduma na haki zao za msingi. Kwa hatua zote hizo, Sisi Viongozi wa Madhehebu ya Dini Mkoa wa Dodoma tunamuunga mkono Mheshimiwa Rais Magufuli, Alimaliza Alhaji Bura

Padiri Onesmo Wisini kutoka Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dodoma amesema kundi lao la Viongozi wa kiroho lina idadi kubwa ya watu na kuwa uamuzi wa Mkuu wa Mkoa Dkt. Mahenge kukaa chini na kuwashirikisha viongozi wa Dini linaifanya Serikali kuwafikia wananchi walio wengi zaidi kwa urahisi na kuomba kuwa utaratibu huu uendelee na uwe wa mara kwa mara. Aidha, wamemshauri Mkuu wa Mkoa kuhakikisha kunakuwa na ushiriki wa Viongozi wa Madhehebu ya Dini na Wazee wa Mkoa kwenye Kamati ya Ushauri ya Mkoa. Viongozi hao wamemuombea Dua Mkuu wa Mkoa Dkt. Mahenge, Mheshimiwa Rais Magufuli na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mkutano kati yake na Viongozi wa Madhehebu ya Dini Mkoa wa Dodoma.



Sheikh wa Mkoa wa Dodoma na Qadhi Mküu wa Mkoa Dodoma ambaye pia ndio Mwenyekiti wa kamati ya Amani na Mahusiano ya Viongozi wa Dini Sheikh Mustwafa Rajabu Shaaban akichangia jambo wakati wa mkutano baina ya viongozi hao na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge (kulia) .



Katikati Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Dodoma Amon Kinyunyu ambaye pia ni Mwenyekiti mwenza wa kamati ya amani na mahusiano Dodoma akikazia jambo wakati wa mkutano baina ya viongozi wa dini na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge (kushoto).

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.