• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MPWAPWA KUNIFAIKA NA BWAWA LA BILIONI 27

Imetumwa : March 2nd, 2023


Serikali imetoa fedha kiasi cha Shilingi bilioni 27.9 kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la Msagali litakalotumika kwa shughuli za kilimo biashara katika Kata ya Ng’ambi na Chunyu, Wilaya ya Mpwapwa, Mkoani Dodoma.

Akikagua maendeleo ya ujenzi huo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema kukamilika kwa bwawa hilo kutasaidia Wilaya ya Mpwapwa na maeneo ya jirani kujishughulisha na kilimo mwaka mzima.

"Ndugu zangu Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuwakomboa wana Mpwapwa kwa kuleta mradi huu mkubwa ambao utakuwa ni mkombozi kiuchumi na kijamii, rai yangu ujenzi huu uzingatie viwango vya ubora na ukamilike kwa wakati" Amesisitiza Mhe. Senyamule.

Bwawa hilo lenye ukubwa wa hekta 1428 sawa na kilometa za mraba 14 litakuwa na ukubwa wa mita za ujazo 92.2 sawa na lita bilioni 92.2 na ujenzi wake umefikia asilimia 30 tangu kuanza kwake miezi minne iliyopita.

Akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa bwawa hilo Mhandisi wa Umwagiliaji Wilaya ya Mpwapwa, Bw. Nuru Simkoko amesema bwawa hilo litakuwa na uwezo wa kumwagilia zaidi ya hekta 3,500 na kunufaisha skimu ya umwagiliaji ya Msagali iliyopo umbali wa kilometa saba kwa kupokea maji kutoka bomba namba mbili ambapo itakuwa ni suluhu ya maji ya uhakika na njia ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatuma Mganga amesema ni matarajio ya Serikali kuwa bwawa hilo litakuwa mkombozi kiuchumi na kuwata wananchi hao kuwa walinzi wa miundombinu ya Serikali inayogharimu fedha nyingini.

“Wakazi wa Mpwapwa muwe tayari kulima kilimo cha mwaka mzima, bwawa hili litakuwa na manufaa kiuchumi, mazingira na afya kwa ujumla” Amesisitiza Dkt. Mganga.

Ujenzi wa bwawa unagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 27.9 na kazi ya ujenzi inafanywa na kampuni ya wazawa ya GNMS Contactors Co. Ltd kutoka Iringa na ujenzi unatarajia kukamilika mwezi Novemba 2023.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.