• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MPWAPWA KUNUFAIKA NA BWAWA LA BILION 27

Imetumwa : June 17th, 2023



Serikali imetoa fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 27.9 kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la Msagali litakalotumika kwa shughuli za kilimo biashara katika Kata ya Ng’ambi na Chunyu, Wilaya ya Mpwapwa, Mkoani Dodoma.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Dodoma Rosemary Senyamule wakati wa siku ya pili ya ziara ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ndugu Daniel Chongolo katika Mkoa wa Dodoma.

Senyemule amesema kukamilika kwa bwawa hilo kutasaidia Wilaya ya Mpwapwa na maeneo ya jirani kujishughulisha na kilimo mwaka mzima.

"Ndugu zangu Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuwakomboa wana Mpwapwa kwa kuleta mradi huu mkubwa ambao utakuwa ni mkombozi kiuchumi na kijamii, rai yangu tuhamikishe mradi huu unatunza ili uweze kutunufaisha sote" Amesisitiza Mhe. Senyamule.

Senyamule amesema kwa Wilaya ya Mpwapwa Serikali imeendea kuleta miradi ya Afya, Elimu na ujenzi wa miundombinu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Barabara na skimu za umwagiliji.

Senyamule amewataka wakazi wa Kingiti kuendea kutunza na kuhifadhi mazingira kwakuwa uhai wa kila kiumbe unategemea mazingira endelevu.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Bw. Daniel Chongolo amekemea vikali uharibu wa mazingira unaofanywa na wakazi wa Kingiti katika Milima ya Guru na Lugundalule na kumwagiza Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama kuchukua hatua kali za kisheria kwa waharibifu wote wa mazingira.

“Hakuna maisha bila kutunza na kuhifadhi mazingira, maisha yetu sote yanategemea hifadhi endelevu ya vyanzo maji, maji ni uhai hivyo tukiharibu vyanzo hivi tunahatarisha uhai wetu wenyewe. Hatuwezi kucheza na maisha ya watu kwa kuruhusi hali ya uharibifu iendelee” Chongolo amekemea.

Bwawa hilo lenye ukubwa wa hekta 1428 sawa na kilometa za mraba 14 litakuwa na ukubwa wa mita za ujazo 92.2 sawa na lita bilioni 92.2. Ujenzi wa bwawa unagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 27.9 na kazi ya ujenzi inafanywa na kampuni ya wazawa ya GNMS Contactors Co. Ltd kutoka Iringa na ujenzi unatarajia kukamilika mwezi Novemba 2023.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.