• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MPWAPWA YADHAMIRA UKUSANYAJI WA MAPATO

Imetumwa : July 8th, 2023

Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa Mkoani Dodoma imedhamiria kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa mwaka huu wa fedha (2023/2024) baada ya kubuni chanzo kitakachoimarisha mapato hayo kwa ukamilifu.

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Sophia Kizigo amesema hayo leo katika Mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo lilijadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia 2022/2023.

Amesema Halmashuri ya Wilaya ya Mpwapwa imenunua kifaa maalumu cha kisasa cha kidijitali (RTK – GPS) kwa gharama ya Shilingi Milioni 37.5 kwa ajili ya upimaji wa viwanja jambo ambalo litaongeza mapato katika halmashauri hiyo na kuwezesha Wilaya hiyo kupima viwanja vingi kwa wakati mmoja.

Akizindua kifaa hicho Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ametoa pongezi kwa Wilaya hiyo kwa kuona umuhimu wa kuwa na mkakati endelevu wa kupanga Wilaya ya Mpwapwa kupitia uuzaji wa viwanja.

“Mwaka huu wa fedha unaoisha mlikusanya mapato kwa asilimia 92 niwapongeze sana ni Imani yangu kuwa asilimia 8 iliyobaki na zaidi itakamilika kupitia mkakati huu mliobuni wenyewe kama chanzo kimojawapo cha mapato. Nimefurahi kwakuwa mmejipanga kutumia  kifaa hiki cha kisasa cha RTK - GPS hii kwa shughuli za upimaji, nasisitiza upangaji na umilikishaji ufanyike ili kuleta iliyokusudiwa tija” Senyemule amesisitiza.

Awali Mhe. Senyamule pia ameshiriki katika mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani kwa lengo la kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu za mwaka 2021/2022) kwa kila Halmashauri.

Aidha, Senyamule ameagiza Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kuhakikisha kuwa hoja zote za ukaguzi zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na zile za Mkaguzi wa ndani, zinashughulikiwa ipasavyo na kupatiwa majibu stahiki ili ziweze kuhakikiwa na kufungwa kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na maelekezo yaliyotolewa na Serikali.

“Mheshimiwa Mwenyekiti na Menejimenti ya Halmashauri hapa Mpwapwa ni lazima mje na Mkakati madhubuti wa kumaliza hizi hoja 53 zilizosalia, iwe ni agenda ya kudumu katika vikao vyenu kujua  hoja ngapi zimemalizika na ngapi bado ili muweze kuwa na mkakati madhubuti wa kusimaliza” Senyamule amesisitiza.

 Senyemule ametoa rai kwa Halmashauri hiyo kuzingatia ipasavyo Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo mbalimbali iliyopo katika uendeshaji wa shughuli za kila siku ili kupunguza hoja za ukaguzi zisizokuwa za lazima.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.