• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MRADI WA RELI YA KISASA YA UMEME SGR MBIONI KUKAMILIKA JANUARY -2024

Imetumwa : November 10th, 2023



Mradi wa reli ya kisasa ya umeme (SGR) unatarajia kukamilika Januari mwakani ambapo unahusisha kipande cha kutoka Morogoro, Dodoma na Makutupora.


Hayo yamebainishwa hii leo Novemba 10, 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa ndani ya Jiji hilo ambapo ametembelea mradi wa Reli ya kisasa ya umeme (SGR ) na Mji wa Serikali Mtumba (Magufuli City). Amesema ameridhishwa na mradi huo ambao mpaka sasa kwa mujibu wa mkandarasi umefikia asilimia 95.7 kukamilika.


Amesema kupitia mradi huo utaongeza kasi ya maendeleo na fursa za kiuchumi ikiwa ni pamoja na kupendezesha mandhari ya jiji la Dodoma ambapo pia ni fursa ya utalii hivyo amewataka wananchi kuchangamkia fursa za kiuchumi


Aidha, amewaagiza wasimamizi wa mradi ambao ni Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuendelea kutoa elimu kwa wananchi wanaozunguka maeneo ya mradi huo juu ya kuchukua tahadhari ikiwemo ya usalama wa mifugo na watu katika eneo la miradi kwa kuhakikisha wanapita maeneo husika ambayo yamewekwa kwa ajili ya matumizi yao ikiwemo vivuko kwa ajili ya usalama.


Akiwa katika Mji wa Serikali Mhe.Senyamule amekagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Wizara na ameonyesha kuridhishwa na kasi ya maendeleo ya miradi hiyo.


Hata hivyo, amewaagiza wakandarasi wa miradi hiyo kuongeza kasi ya ujenzi kwa kuzingatia ubora wa majengo hayo ili kufikia Januari 2024 iwe imekamilika huku akiendelea kusisitiza suala la kupanda miti ili kutunza mazingira.


"Tumekuja leo kutembelea na kuona maendeleo ya miradi ambayo pia ni kivutio cha Utalii ndani ya Jiji letu ambayo yapo katika hatua tofauti tofauti, kuna yaliyofikia asilimia 75 hadi 78 na kuna ya asilimia 99.9, kuna ya asilimia 53 ambapo ya asilimia 75-78 yalitakiwa yawe yamekamilika .


"Nitoe wito kwa wakandarasi waliopata fursa za kujenga, hakikisheni mnatimiza wajibu wenu, punguzeni sababu nyingi kwani tuna amini Changamoto zipo ila tatueni kwa haraka ili kukamilisha majengo haya kwa wakati husika " Ameeleza Mhe. Senyamule


Kwa Upande Wake, Meneja wa Ujenzi (TBA ) Injinia Manasseh Shekalaghe, amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa watasimamia wakandarasi kwa ukaribu zaidi ili ikifika Januari watumishi wote waweze kuhamia Mtumba .



Ziara hiyo imehusisha kutembelea maendeleo ya mradi wa Reli ya kisasa ya umeme ( SGR) ambapo ametembelea katika jengo la abiria Mkonze , karakana na kituo cha kushushia mizigo Ihumwa jijini Dodoma. Kwenye Mji wa Serikali ametembelea Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Wizara ya Utumishi, ziara hii imekua ni mwendeleo wa Mkuu huyo kutembelea miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa jijini Dodoma.





Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.