• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MRADI WA REST WAZINDULIWA DODOMA

Imetumwa : January 16th, 2023

MRADI WA REST WAZINDULIWA DODOMA

Mkoa wa Dodoma umezindua rasmi mradi unaoshughulikia masuala ya afya ya uzazi kwa vijana, wanawake na watoto unaojulikana kama Reproductive Equity Strategic (REST) unaoendeshwa na shirika lisilo la Kiserikali la Deutsche Shiftung Weltbevolkerung (DSW) - Tanzania ambao utafanya kazi kwenye Wilaya tatu za Mkoa ikiwa ni pamoja na Dodoma mjini, Bahi na Mpwapwa. Mradi huo umezinduliwa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Rosemary Senyamule kwenye kikao kilichofanyika ukumbi wa jengo la Mkapa.

Akizindua mradi huo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema Serikali ya Awamu ya Sita imetoa kipaumbele katika sekta ya afya ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu yake ili kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma bora ya afya.

“Matokeo ya sensa ya mwaka 2022 yanaonyesha kuwa Tanzania ina jumla ya hospitali 676, vituo vya afya 1,466 na zahanati 7, 965. Tanzania Bara pekee ina hospitali 662, vituo vya afya 1,430 na zahanati 7,680 na mkoa wetu wa Dodoma una vituo vya afya 69 na zahanati 402. Hivyo ni muhimu sana kuendelea kuhamasisha wananchi hususan wakina mama wajawazito kutumia vituo vya afya kwa ajili ya kupata huduma, mpango wa Serikali ni kutokomeza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga ifikapo mwaka 2025” Amesema Mhe. Senyamule

Mheshimiwa Senyamule ametoa rai kwa waratibu na watekelezaji wa mradi huu kuweka malengo ya kufika kata nyingi zaidi za Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi.

“Mradi huu unafanya kazi kwenye Kata 17 tu za Halmashauri hizi tatu, wakati Dodoma ina kata nyingi zaidi, tupange mkakati wa kuzifikia kata nyingi zaidi za mkoa ili muwe mfano wa kuigwa na kuvutia wengi zaidi kuwekeza Dodoma. Nitoe rai, mkafanye kazi kwa ufanisi mkubwa maana tunataka kila unachokifanya Dodoma, kifanyike kwa ufanisi kwani tunakwenda kuifaharisha Dodoma kwa mradi huu” Ameongeza Mhe. Senyamule

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la DSW Bw. Peter Owaga, amesema “mradi huu unatekelezwa kwenye mikoa minne ya Tanzania ambayo ni ambayo ni Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza na kwa mkoa wa Dodoma unatekelezwa katika Wilaya tatu ikiwemo Dodoma mjini, Bahi na Mpwapwa chini ya mashirika ya DOYODO, WOWAP na FAEAF wakiongozwa na Shirika la DSW Tanzania

Lengo la mradi huu ni kuwajengea uwezo asasi zisizo za kiserikali na kusaidia wanawake na wasichana wanapata na wanatumia huduma za afya ikiwemo afya ya uzazi ili kuleta ustawi wao na kuweza kutimiza matarajio na malengo ya maisha yao. Mradi huu pia utasaidia utekelezaji wa sera na miongozo mbalimbali ya afya ya uzazi ikiwemo kupinga unyanyasaji wa kijinsia na ukatili dhidi ya wanawake, wasichana na watoto.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.