• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MTI WANGU BIRTDAY YANGU DESEMBA, YAPANDA MITI 400 JK SQURE

Imetumwa : December 19th, 2024

Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS

Kampeni ya Mti,Wangu Birthday Yangu inayoendeshwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, kwa mara nyingine imefanikiwa  kuwakutanisha baadhi ya Wakazi wa Mkoa wa Dodoma, Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa  pamoja na baadhi ya Watumishi wa Taasisi za Serikali zilizopo katika mkoa huu  kama TFS,TANESCO,TANROADS, TANAPA,TARURA waliozaliwa mwezi wa 12, maarufu kama 'Team December ' kupanda miti hapo jana Desemba 18, 2024, huku wakisindikizwa na watumishi wenzao kutoka kwenye Taasisi hizo,ambapo kwa umoja wao walifanikiwa kupanda miti 400 pembezoni mwa barabara ya kuzunguka eneo la JK. Squre lililopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa lengo la kupendezesha mandhari yake kwani linatarajiwa kuwa ni eneo  la kupumzikia na kufanyia hafla mbalimbali.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo inayofanyika kila mwezi, Muasisi wa Kampeni hiyo inayounga mkono kampeni mama ya ‘Kijanisha Dodoma’ Katibu Tawala Mkoa  Bw. Kaspar K. Mmuya amesema;

“Leo hii tumepanda miti 400 na miti ile tumepanda kimkakati, pembezoni mwa barabara, na itakua kama kiashiria kwamba huku kuna kitu hivyo ukuaji wake utakuwa na ukomo   ili kupendezesha hili eneo. Tunataka hapo baadae litumike kwa shughuli mbalimbali bila kuweka mahema kwani kutakua na kivuli cha kutosha.” Bw. Mmuya.

Kamishna Mwandamizi Msaidizi na Meneja wa rasilimali za nyuki kutoka Wakala wa Uhifadhi wa Misitu Tanzania (TFS) Bw. Hussein Msuya, amesema miti ni uhai kwani hewa ya oksijeni tunayoitumia inatoka kwenye miti, pia ni rasilimali kwa ajili ya nyuki ambao wanatumia maua kuzalisha asali hivyo ukiondoa miti, umeondoa nyuki duniani.

Aidha,Kamishna Msaidizi Mwandamizi Jeshi la Uhifadhi, Mkuu wa Ofisi ya Mahusiano TANAPA Dodoma Dkt.Noelia A. Myonga amesema amefarijika na zoezi la kukijanisha Dodoma kwani linakumbusha uumbaji wa Mungu ambaye aliumba mazingira yote kisha mwanadamu ili aweze kuyasimamia na kuyatunza mazingira hayo.

Naye, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Winiesta Saria alisema kupanda miti ni ajenda ya Chuo hicho, na  siku ya Jumamosi Desemba 14, 2024 walipanda miti 6,500 lengo likiwa ni kukizungushia chuo uzio wa miti ili isaidie mipaka, matunda pamoja na kuongeza kiwango cha mvua kwa siku za usoni,kwani kwa sasa mvua zinanyesha Dodoma kwa siku 35 tu kwa mwaka hivyo kupanda miti kutasababisha mvua kuongezeka.

&&&

#dodomafahariyawatanzania                                 #keroyakowajibuwangu  #mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.