• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MWENGE WA UHURU 2025 MKOA WA DODOMA KUPITIA MIRADI YA BILIONI 61.1

Imetumwa : April 19th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 Mkoa wa Dodoma ambao utapokelewa siku ya Jumapili Aprili 20, 2025, unatarajiwa kukimbizwa umbali wa Kilometa 1350 na kupitia miradi yenye thamani ya shilingi 61,105,007,015.00 iliyopo katika Halmashauri nane (08) za Mkoa.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule katika taarifa yake kwa vyombo vya habari juu ya mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 katika Mkoa wake aliyoitoa leo Aprili 19, 2025 kwenye ukumbi wa Ofisi yake jengo la Mkapa Jijini humu.

“Mwenge wa Uhuru 2025 utakimbizwa umbali wa Km. 1,350, utapitia miradi 56 kati ya hiyo miradi 16 itawekewa mawe ya msingi, miwili itafunguliwa, 24 itazinduliwa na 14 itatembelewa. Miradi yote ina thamani ya shilingi 61,105,007,015.00 katika mchanganuo ufuatao, Serikali kuu Bil. 39.358 Halmashauri Bil. 3.615 Wafadhili Bil. 5.997 na nguvu za wananchi Bil. 12.133”

Aidha, Mhe Senyamule ametumia fursa hiyo kuwaalika wananchi wote wa Mkoa wa Dodoma kujitokeza kwa wingi kwenye mapokezi ya Mwenge wa Uhuru katika maeneo yote ambayo utapita kwani hii ni fursa nzuri kwao kuonesha umoja, kutangaza maendeleo yanayoendelea ndani ya Mkoa na kazi kubwa ambayo imefanywa na Serikali kwenye Mkoa.

Mwenge wa Uhuru 2025 Mkoani Dodoma unatarajiwa kupokelewa kimkoa kwenye uwanja wa CCM uliopo Kata ya Kibaigwa, Wilaya ya Kongwa, utapita Wilaya zote 7 na Halmashauri 8 ambapo tarehe 20, utakimbizwa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Aprili 21 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Aprili 22 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba.

Kadhalika, Aprili 23 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Aprili 24 utakimbizwa katika Halmashauri ya Mji Kondoa, Aprili 25 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Aprili 26 Halmashauri ya Jiji la Dodoma na tamati ya mbio hizo ni Aprili 27 ambapo utakimbizwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwampwa.

Kaulimbiu: “Jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu”


#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

#karibumwengewauhuru2025mkoawadodoma

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.