• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mwenge wa Uhuru Kuwasili Mkoani Dodoma,kukimbizwa KM 1162

Imetumwa : August 16th, 2022

Mwenge wa Uhuru leo umeingia Mkoa wa Dodoma , Makao Makuu ya Nchi ambapo utakuwa Mkoani hapo kwa kipindi cha Siku nane kuanzia tarehe 16/8 hadi 23/8/2022.

Akizungumza baada ya kupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Peter  Serukamba,Mkuu wa  Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amesema mwaka huu 2022 , Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Dodoma utapita katika Wilaya saba na halmshauri nane za mkoa wa Dodoma ambazo ni Bahi, Dodoma Jiji, Chemba, Kondoa (V), Kondoa Mji, Chamwino, Mpwapwa na kumalizia Kongwa. 

Ukiwa Mkoani Dodoma Mwenge wa Uhuru utakimbizwa kilometa 1162 na utapitia jumla ya miradi 39 ambapo kati ya miradi hiyo 39, 19 itawekewa mawe ya msingi, 10 itazinduliwa na 10 itatembelewa.

Akileleza thamani ya miradi hiyo Mhe. Senyamule amesema kuwa miradi hiyo ina thamani ya Tsh.14,156,615,332/-. "Miradi hii imetekelezwa kwa ushirikiano mkubwa uliopo kati ya Serikali Kuu, Halmashauri, Wananchi na Wadau wa Maendeleo".Amesema RC Senyamule.

Mhe. Senyamule amemshukuru, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuupatia  mkoa wa Dodoma fedha za miradi mingi ya kimkakati na mikubwa kwenye sekta ya miundo mbinu, Ujenzi, Usafirishaji, Kilimo, Elimu, Afya,biashara na huduma mbalimbali.

Aidha Mkuu wa Mkoa amewapongeza na kuwakaribisha wakimbiza mwenge kitaifa Mkoani Dodoma na kuahidi kuwapa ushirikiano wote wataohitaji ili kufanikisha kazi yao.

Akitikia ukaribisho huo Kiongozi wa Mbio za  Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Sahili Nyanzabara Geraruma ameeleza kuwa mwaka huu Ujumbe wa Mwenge wa Uhuru unasema Sensa ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo:Shiriki Kuhesabiwa, Tuyafikie Malengo ya Taifa. Aidha Bw. Geraruma ametaja Jumbe mbalimbali za Mwenge zitakazo wakumbusha wanchi kuhusu kuzuia rushwa, lishe bora msingi wa uchumi imara, zingatia usawa tokomeza ukimwi na magongwa ya mlipuko pamoja na ziro malaria inaanza na mimi nachukua hatua kutokomeza na dawa za kulevya -( tuelimishane juu ya tatizo la dawa za kulevya , ili kuokoa maisha.

Mwenge wa Uhuru uliwasili Mkoani Dodoma ukitokea Mkoani Singida ambako ulikimbizwa kuanzia tarehe 09/8-15/8/2022.

Mwisho

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.