• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MWENYEKITI CHEMBA ATAKIWA KUCHUNGUZA KUSUASUA KWA MRADI WA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA

Imetumwa : November 18th, 2022


"Sura ya Ujenzi wa miradi kwa Chemba sio nzuri, tuamue kubadilika kwani tulikaa tukaelekezana mara tu fedha zilipotoka. Hakuna aliyekuja ofisini kwangu kutoa malalamiko ya fedha kuchelewa. Watumishi wa Serikali tupo juu ya vikwazo, tunatakiwa kukabiliana na changamoto zote miradi hii ikamilike kwa wakati"

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule alipotembelea na kukagua miradi ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule tatu za sekondari za Halmashauri ya Chemba ambazo ni Mondo na Chemba pamoja na shule ya sekondari inayojengwa kwa mradi maalumu wa SEQUIP shule ya sekondari ya Churuku.

Katika mradi wa vyumba vinne vya madarasa katika sekondari ya Mondo iliyopokea kiasi cha Shilingi milioni 80 , Mkuu wa Mkoa hakupendezwa na kasi ya Ujenzi wa vyumba hivyo na kumtaka Mkuu wa shule kujipanga na kamati yake kuumaliza mradi kwa wakati.

Kadhalika, shule ya sekondari ya Chemba imepokea Shilingi Milioni 120 kutekeleza ujenzi wa madarasa 6, ofisi 1, viti 100 na meza 300 nayo bado hali ya Ujenzi wake haijafikia kiwango cha kukamilisha kwa kipindi kilichokua kwenye makubaliano ingawa Mkuu wa shule ameahidi mpaka kufikia Desemba 5 tayari atakabidhi mradi.

Kwenye shule ya sekondari ya Churuku iliyo chini ya mradi maalumu wa SEQUIP, ambayo imepokea Shilingi Milioni 600, mpaka Sasa mradi haujakamilika na fedha iliyotolewa imekwisha na Mkurugenzi ameomba kuongezea kiasi cha Shilingi Milioni 40 kumalizia madarasa na vyoo kwa ajili ya usajili na kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwakani ingawa kwa tathmini bado zinahitajika Milioni 156 kukamilisha mradi mzima kwa kiwango kilichobaki chenye kukidhi mahitaji.

"Majimbo matano shule zimekamilika bado majimbo 6 tu kwenye baadhi ya Halmashauri, wote tumepewa fedha zinazofanana sasa ukiniambia zinahitajika Milioni 156 kumalizia hapo kuna jambo halijakaa sawa. Mwenyekiti fanya uchunguzi kuangalia nini tatizo" RC Senyamule

Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe. Simon Chacha amesema kuwa amepokea maelekezo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa na ameahidi kuyasimamia kwa watendaji wote na amewataka watendaji wake kila mmoja anayehusika na mradi asikae ofisini kuanzia Juma lijalo bali awe kwenye eneo la ujenzi.

Akitoa tathmini yake juu ya maendeleo ya miradi yote kwa ujumla, Mkandarasi wa Mkoa Bi Happiness Mgalula amesema hali ya ujenzi inaridhisha licha ya kuwa nyuma ya muda kwa mujibu wa ratiba hivyo viongozi wanapaswa kuongeza usimamizi na ufuatiliaji wa ujenzi ili miradi yote iweze kukamilika kwa wakati waliokubaliana.

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.