• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

"Naomba Muwamini Polisi na Kuwapa Ushirikiano"-RC- Mtaka

Imetumwa : June 5th, 2022

“Naomba Muwamini Polisi na Kuwapa Ushirikiano”- RC – Mtaka 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka, ameyasema hayo wakati wa Mkutano wa hadhara Uliofanyika hivi karibuni katika Shule ya Msingi Kisasa, Kata ya Kisasa /Makulu. Mkutano huo ni mwendelezo wa mikutano ambayo imekuwa ikifanywa na Mkuu wa Mkoa pamoja na wakuu wa Wilaya yenye lengo la  kusilikiza kero za wananchi na kuzungumzia hali ya ulinzi na usalama katika maeneo yao. Mhe. Mtaka ambaye ndie alikuwa mgeni rasmi wa mkutano huo aliambatana na Kamati ya ulinzi na usalama Mkoa, Wilaya, Kamanda wa Polisi Mkoa, Mbunge wa Dodoma mjini, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mkurugenzi wa Jiji, Meya, Diwani wa Kata ya Makulu, wenyeviti wa mitaa, watendaji kata pamoja na wakazi wa Kisasa.

Licha ya kuzungumza na wananchi, Mhe. Mtaka amekua akifanya mikutano na vikao vya aina hii  kwa makundi mbalimbali yakiwemo Jeshi la Polisi, madereva wa pikipiki maarufu kama Bodaboda na Bajaji pamoja na  wenyeviti wa  Serikali za  mitaa na Kata.

Mhe. Mkuu wa Mkoa alitoa fursa kwa wananchi na wakazi wa Kisasa kueleza kero zao na hasa zile zinazohusu masuala ya kiusalama kwani eneo hilo limekuwa likigubikwa na matukio mengi ya kiuhalifu na mengine ambayo ni ya kudhalilisha utu wa watu.Takribani wananchi 40 wa Kisasa ambao kwa njia moja ama nyingine ni wahanga wa vitendo vya kihalifu vinavyofanyika katika maeneo yao, walipata nafasi ya kubainisha baadhi ya vitendo vya kihalifu vinavyofanywa na vijana wadogo wenye umri kati ya miaka 14 mpaka 20 wanaojiita "panya kaloa". Vijana hawa wamekua kero kubwa kwa wakazi wa Kisasa kwani wanafanya matukio ya unyang'anyi, kuvunja nyumba na hata ubakaji wakitumia silaha za jadi na bunduki.Hali hii inawafanya wananchi kuishi kwa hofu kwani hawajui hatma ya kesho yao pamoja na mali zao huku wakilalamikia ukosefu wa kituo cha Polisi cha kudumu kwani kilichopo ni kidogo na cha muda tu.Wananchi hao walitaja uwepo wa maeneo yasiyoendelezwa kuwa ni chanzo kingine cha kuchochea uhalifu zaidi.

Pamoja na hali tajwa, wananchi hao walibainisha kuwa kuna baadhi ya wanafunzi ambao wakitoka majumbani kwao wanaaga kuwa wanaenda shule ila kiuhalisia hawafiki shuleni na badala yake hufanya kazi ya kuwakaba watu.

Akizungumza baada ya kusikiliza kero za wananchi hao, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.  Anthony Mtaka amesema Ulinzi na usalama ni suala la kila mmoja wetu,hivyo kila mmoja anajukumu la kutoa taarifa endapo anaona kiashiria chochote cha kutishia amani. Mhe.Mtaka amewataka wananchi kuwa na Imani na jeshi la Polisi na kuwapa ushirikiano, wananchi washirikiane nalo kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi mitaani kwa utaratibu mzuri. Aidha Mhe. Mtaka ametaja umuhimu wa kuanzisha Wilaya maalum za Kipolisi kwani Mkoa umekua kwa kiwango cha kuridhisha.

 Akizungumzia suala la utoro shuleni  Mhe. Mtaka, amewaasa wazazi na walezi kufuatilia mwenendo wa Watoto wao wanapokwenda shule kwani kutokufanya hivyo ndio kunapelekea kuwa zao la panya road na panya kaloa ambao wanatishia hali ya usalama wa maisha ya watu. Aidha Mkuu wa Mkoa amewataka  wananchi kuwapeleka watoto wahalifu kwenye mikono ya Sheria kwani ipo Sheria inayoshughulikia uhalifu Kwa watoto.

Mhe Mtaka ameshauri ufungaji wa Camera za ulinzi majumbani na kwenye maeneo ya Biashara pamoja na kituo Mama cha Bodaboda, Kisasa sheli. Pia amewataka viongozi wa dini kuongelea suala la maadili kwa vijana wakati wa Ibada  zao kwani hiyo itasaidia kuwarekebisha. Mkuu wa Mkoa  amewataka viongozi hao kufanya Ibada kwa utaratibu ili kuepuka  kuwa kero ya kelele kwa nyumba za majirani. “Dini tunazipenda na kuziheshimu sana , lakini heshimuni  makazi ya watu.Hali kadhalika na maeneo ya Biashara za vinywaji punguzeni kelele za muziki wakati wa usiku ili kuleta utulivu mitaani”.Amesisitiza Mtaka.

Mhe. Anthony Mavunde ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, amesema, uhalifu unaojitokeza katika maeneo ya Jiji la Dodoma unatokana na maendeleo makubwa ya kukua kwa Mkoa hivyo ameshauri vituo vya waendesha Bodaboda vinavyofanya kazi  saa za usiku visajiliwe ili kuepuka uhalifu kwa abiria pia ameahidi kuchangia tofali 2,000 na mifuko 50 ya Saruji kwenye Ujenzi wa kituo cha kudumu cha Polisi ambacho wananchi wameahidi kujitolea nguvu zao.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Bw. Jabir Shekimweri, amewataka wananchi wa Kisasa na Dodoma kwa ujumla kutambua kwamba jukumu la ulinzi binafsi ni la kila mmoja hivyo wazazi na walezi watoe hamasa kwa vijana wao waliomaliza elimu kujiunga kwenye ujasiriamali au vikundi vya ulinzi shirikishi na sio kufanya uhalifu ambao utapelekea kuharibu kabisa maisha yao. Mhe Shekimweri   amewataka wale wenye uwezo wafunge camera za ulinzi (CCTV) kwenye majumba yao.

Akijibu hoja zilizotolewa na wananchi ikiwemo ukosefu wa kituo cha Polisi cha kudumu katika eneo hilo pamoja na uwepo wa maeneo yasiyoendelezwa ambayo yamegeuka vichaka na maficho ya wahalifu, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Bw. Joseph Mafuru, alisema kuwa eneo kwa ajili ya Ujenzi wa kituo cha Polisi lipo na endapo wananchi wapo tayari kijitolea kwa ujenzi, kibali kitatolewa. Pia kuhusu uwepo wa maeneo ambayo hayajaendelezwa, alisema Jiji litawanyang'anya wamiliki watakaobainika kwani kwa mujibu wa Sheria, eneo linaponunuliwa linatakiwa kuendeleza ndani ya kipindi cha miezi 36.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. Martin Otieno, aliwaambia wananchi wa Kisasa kulinda amani kwani bila amani hakuna maendeleo yatakayopatikana katika eneo hilo. Pia amewataka kutoa ushirikiano katika kuanzisha ulinzi shirikishi na ambao hawataweza kushiriki basi wawawezeshe wale watakaojitolea na mwisho aliwataka wananchi kuwa wepesi kutoa taarifa za kweli za uhalifu kwani hii itasaidia kufanyika uchunguzi wa haraka.

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.