• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

"NATARAJIA MABADILIKO MAKUBWA KWENYE ELIMU"RC SENYAMULE

Imetumwa : November 10th, 2022

“Dodoma tuna upungufu mkubwa wa miundombinu ya elimu, utoro, mimba na ndoa za utotoni. Mkoa wa Dodoma ni Mkoa wa tatu kwa masuala ya mimba za utotoni na wanafunzi kuolewa.Aidha pamoja na changamoto hizo bado tuna changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa. Katika wilaya ya Chamwino tuna upungufu vyumba vya madarasa 1104 kwa  Shule za msingi na na madarasa 94  kwa shule za sekondari.Baada ya mapokezi ya Tsh.6.78 bln changamoto ya madarasa 94 ya sekondari kwa wilaya ya Chamwino itaisha.”

Kuhusu changamoto za utoro darasani , mimba na ndoa za utotoni   naagiza vifanyike vikao vya ngazi za elimu na wadau wakiwemo walimu, ODC, wazazi na wanafunzi, vikao hivyo vifanyike kila kata. Kila kata mjitathinmi kuhusu masuala ya elimu nataka nione malengo ya kila kata, katika mabadiliko makubwa ninayoyatarajia. Katibu Tawala Msaidizi Menejimenti ya Ufuatiliaji na Ukaguzi, nataka nipate ripoti ya utoro kila Ijumaa.Na kabla ya kila ziara ya eneo husika” RC Senyamule.

Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo wakati wa ziara yake wilayani Chamwino ambapo ameambatana na Katibu Tawala Mkoa Dkt. Fatuma Mganga, Kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa pamoja na viongozi wa idara mbalimbali za Mkoa. Ziara ambayo ameifanya akiwa na lengo la kujitambulisha, kusikiliza kero za wafanyakazi, madiwani na wananchi wa Chamwino na hatimae kuwapatia maelekezo ya Serikali.

Akizungumza na watumishi pamoja na madiwani wanaowawakilisha wananchi katika kata zao. Miongoni mwa kero zilizowasilishwa mbele ya Mkuu wa Mkoa ni; soko la zabibu kufanya vibaya mwaka huu, baadhi ya wakulima kutokulipwa kwa wakati,kero ya wanyamapori hususan tembo wanaofanya uharibifu wa makazi na mazao, kukosekana kwa alama za matuta kwenye baadhi ya barabara za TANROADS, changamoto ya maji, daraja la Manchali n.k

Kero hizo zimepata majibu kutoka kwa wataalamu wa idara husika. Aidha baada ya majibu ya wataalam, Mkuu wa mkoa amewaeleza wananchi wa Chamwino kuwa

“Wizara ya kilimo imejipanga kupambana na soko la zabibu kwa kutenga kiasi cha fedha kwa ajili ya kununua matenki makubwa ya kuhifadhia mchuzi wa zabibu hivyo tunategemea mwaka kesho tatizo litakwisha. Pia TAHA ambao wanajihusisha na usafirisahji wa mazao nje ya nchi kwa ajili ya masoko, wamefanya kikao na wadau wa zabibu na suala hili wamelibeba kulifanyia kazi” RC Senyamule amesema

Aidha, Mkuu wa mkoa ameongea na watumishi wa Halmashauri ya Chamwino na kuwapa maagizo ya Serikali ambayo ya yamegusa suala la elimu, kilimo, miradi pamoja na utawala bora.

Akizungumza Katibu Tawala Dkt.Fatuma Mganga amewapongeza Halmashauri ya Chamwino kwa ukumbi mzuri,hongereni sana kwani madhari inapendeza. Kuhusiana na Makusanyo ya mapato Dkt, Mganga amewapongeza kwa lengo lao la kuongezeka kutoka Tsh. 2.7bln kufikia Tsh.3.0bln na kuwapa angalizo la  mapato kuendana na ukubwa wa eneo na shughuli za kibiashara.

“Ukubwa wa eneo ni ukubwa wa fursa hongera hivyo ingefaa kama mngeongeza  kiwango cha lengo la ukusanyaji mapato angalau mfike 5bln, kwani mna fursa nyingi, pia mmepata bwawa moja.Inabidi muwe na mikakati mizuri sana ya kutumia hilo bwawa la Membe.Nimesikiliza baadhi ya maswali ila mengine ni ya utekelezaji tu mfano suala la maji,tutumie rasilimali kwa uzuri zaidi tumieni hizo gata kuvuna maji ya kutosha hospital.Tukusanye mapato vizuri na kwa mapato hayo tunaweza kuchimba kisima cha hospital.Tusihamishe tatizo RUWASA.Tuwashirikishe wananchi”.Amesema Dkt. Fatuma Mganga.

Sanjari na hayo Mkuu wa Mkoa pamoja na ujumbe wake wametembelea mradi wa shamba la mfano la zabibu lililopo eneo la Chinangali II, shamba linalotarajiwa  kulimwa kwa mfumo wa “block farming” kwa kutumia eneo lenye ukubwa wa ekari 600 ambapo tayari ekari 300 zimesafishwa kwa ajili ya kuanza kilimo Novemba mwaka huu.

Mhe. Senyamule amewataka Halmashauri ya Chamwino kuitunza imani ya Serikali kwani shamba hili ni uwekezaji mkubwa na ni utalii tosha kwa Wilaya na Mkoa kwa ujumla.

“Nimefurahi kufika hapa kujionea uwekezaji huu na niwaahidi kwamba mkoa tutashirikiana kwa karibu kufuatilia maendeleo ya shamba hili kwani tunategemea uchumi wa mkoa, Halmashauri na wa mtu binafsi utapanda kupitia uwekezaji huu” RC Senyamule

Akisoma taarifa ya uwekezaji huu, Mwenyekiti wa Bodi ya CHABUMA AMCOS LTD ambaye ndiye msimamizi wa shamba hilo la uwekezaji Bw. David M. Mwaka, amesema

“Tunategemea kulifanya shamba hili kuwa la mfano na la kitalii pia kwani kwa sasa tuna hekari 600 ambazo tayari tuna hati miliki na tunalilima kwa awamu mbili, ya kwanza ina hekari 295 na ya pili ina ekari 300,ambapo hekari 5 zitatumika katika ujenzi wa Ofisi. Tumepokea mkopo wa kufufua shamba hili wenye jumla ya Shilingi 1,247,436,179 tunamshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kulifanya zao la zabibu kuwa miongoni mwa mazao ya kimkakati na alama ya Mkoa wa Dodoma” Bw. Mwaka

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.