• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

PSSF WAUNGA MKONO JUHUDI ZA MHE.RAIS KYUONGEZA MIUNDOMBINU YA ELIMU

Imetumwa : February 28th, 2025

Na.Francisca Mselemu

       RS Dodoma.


Kuelekea siku ya Wanawake Duniani,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Rosemary Senyamule  amewashukuru PSSSF kuunga mkono kazi kubwa anayoifanya Mhe. Rais Daktari Samia Suluhu Hassan ya kuendeleza Sekta ya Elimu.

.

Mhe. Senyamule ametoa shukrani hizo leo  Februari 28,2025 wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya mfano na   madawati  kwa Shule Mpya ya Sekondari Mayamaya, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku hiyo kwa Watumishi Wanawake wa Mfuko huo wa hifadhi ya Jamii.


Hafla ya makabidhiano  imefanyika katika uwanja wa Shule hiyo iliyopo katika Kijiji cha Mayamaya,kata ya Zanka, wilayani Bahi.


Akizungumza wakati wa hotuba yake,Mhe. Senyamule amesema,

"Msingi wa kukutana hapa ni wenzetu PSSSF  ambao wamekuwa na dhamira ya dhati ya kuja kuungana na  sisi Mkoa wa Dodoma,Wilaya ya Bahi kuongeza miundombinu ya elimu.Lakini pia msingi wake ni Wanawake,tunafahamu kuwa tarehe 08,03 kila mwaka kunakuwa na maadhimisho  ya siku ya Wanawake Duniani ambayo mara nyingi huwa inaanza kuadhimishwa tangu tarehe 01,03.



Mhe. Senyamule ameeleza sababu ni kwa nini mwaka huu Wanawake washeherekea kipekee  siku hiyo."Tunapokwenda kusheherekea hii miaka 30 tangu Mkutano wa Beijing ,tunalo jambo la kusheherekea,jambo la kipekee sana,kwanza Rais wetu ni Mwanamke ambaye katika historia ya Miaka 63 ya Uhuru,awamu hii,tunaye Rais Mwanamke,kikubwa zaidi,sio tu kuwa ni Mwanamke,lakini ni kuwa kazi anayoifanya ni kazi ya kutukuka,kazi ya kuthaminiwa,kazi ya kuheshimiwa na kupigiwa mfano na mtu yeyote.


Mhe Rais kama Mwanamke,kama Jemedari Mkuu na kama Kiongozi wa Nchi,ameitendela haki nafasi yake kwa kufanya mambo makubwa sana katika historia ya Nchi yetu ya Tanzania" Amesema Mhe. Senyamule


Katika hatua nyingine, Mhe Senyamule amewapongeza Watumishi Wanawake wa PSSSF kwa kuona sababu ya kuadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada katika Shule hiyo,huku akitoa wito kwa Wanawake wengine kujifunza kutoka kwa Wanawake hao  ambao badala ya kufikiri kusheherekea kwa kushona sare na kwenda maeneo ya starehe,wameona washeherekee kwa kutoa,tena kutoa ambako kutagusa maisha ya watoto.


Shule ya Sekondari Mayamaya ilianza kujengwa mwaka 2024, hadi sasa vyumba vinne(4) vya madarasa pamoja na ofisi moja (1) vimekamilika, matundu 13 ya vyoo yako katika hatua ya umaliziaji.PSSSF imechangia jumla ya shilingi milioni ishirini na nane ( 28,000,000) kwa ajili ya kuendeleza shughuli za ujenzi pamoja na utengenezaji wa Madawati.




#dodomafahariyatanzania

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.