• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

"RAIS AMEWAPENDELEA MACHINGA WA DODOMA"RC SENYAMULE

Imetumwa : September 15th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mhe. Rosemary Senyamule ametoa pongezi nyingi kwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kiasi cha Shilingi Bilioni Sita kuchangia ujenzi wa soko la litakalotumiwa na wafanyabiashara wadogo wadogo mkoani Dodoma maarufu kama Machinga. Soko hilo limejengwa Jijini Dodoma katika eneo la barabara ya  Bahi ..

Mhe. Senyamule amefanya ziara ya kutembelea soko hilo  hivi karibuni lengo likiwa kukagua marekebisho yaliyotokana na changamoto alizoziona mara ya kwanza alipokwenda kutembelea eneo hilo ambapo alitoa maagizo ya kurekebishwa kwa changamoto hizo ili hatimaye Machinga waweze kuhamia rasmi katika soko hilo.

“Nawashukuru Machinga wa Mkoa wa Dodoma kwa ushirikiano mliotupatia tangu mwanzo wa ujenzi wa soko hili mpaka sasa tunapokwenda kuhitimisha. Mkoa ulikua na ndoto ya kuanzisha jambo hili, tunashukuru kwani  watu wa kuitimiza ndoto hiyo mumepatikana” Mhe. Senyamule

Aidha, Mkuu wa Mkoa, ametoa maagizo kwa Halmashauri ya Jiji kuendelea kukamilisha usajili wa wafanyabiashara watakaohitajika kuwepo sokoni hapo huku akiwataka kuhakikisha marekebisho mengine madogo madogo aliyoyaona yanarekebishwa pia.

“Nawashukuru Halmashauri ya Jiji kwa kuzifanyia kazi changamoto zilizojitokeza lakini pia niwaombe mujaribu kuboresha mahali hapa kwa kuweka miundombinu ya walemavu kwani haipo hapa, hii itasaidia kundi hilo pia kuweza kufika hapa na kupata huduma” Ameongeza.

Naibu Meya wa Jiji la Dodoma Bw. Jamal Yaredi, amekiri kupokea maelekezo yote na kuahidi kuyafanyia kazi. Pia alizungumzia suala la usafi wa soko hilo pindi litakapoanza kufanya kazi kwa kusema kuwa, wamejidhatiti kusimamia suala la usafi sokoni hapo kwani tayari sheria ndogo ndogo za usafi zimewekwa na atakayekiuka atalipa faini.

Akizungumza kwa niaba ya Machinga, Afisa Habari wa Machinga Dodoma Bw. John Mbingo, ameishukuru Serikali kwa kuthamini mchango wa Machinga wa Dodoma kwani heshima hii imetolewa kwa Mkoa huu tu. Ameongeza kuwa soko hili litakua la kitalii zaidi kwani watu kutoka ndani na nje ya Dodoma watakuja kutembea na kujifunza hapa.

Naye Mwenyekiti wa Machinga Dodoma, Bw. Bruno Mponza, ametoa shukrani zake kwa Serikali ya Mkoa kwa ushirikishwaji mkubwa uliopo tangu mwanzo mpaka hitimisho la ujenzi wa soko hilo. Ametoa rai kwa machinga wenzake kulitunza soko hilo ili lionekane jipya kila siku kwani Serikali imewajengea miundombinu rafiki ili waweze kuwa matajiri hivyo wasiangushe juhudi hizo.

Soko la Machinga linalotarajiwa kuanza kazi hivi karibuni, limejengwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kufuatia maagizo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kuwataka wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama machinga watengewe maeneo maalumu ya kufa nyia biashara kwa kwa kuwa na maeneo hayo itasaidia sana miji  kuwa safi. Soko hilo limegharimu zaidi ya shilingi Bilioni 9.5 na linatarajia kubeba machinga zaidi ya 3500

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.