• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RAIS SAMIA AYAGUSA MAKUNDI MAALUM DODOMA

Imetumwa : March 24th, 2025

Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa zawadi kwa Makundi maalum hususan watoto wanaoishi kwenye Makao pamoja na shule maalum zinazopatikana katika Mkoa wa Dodoma ambazo zimekabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule.



Akikabidhi zawadi hizo, katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma eneo la Njedengwa, Jijini Dodoma Mhe. Senyamule amewataka wazazi kuwajibika kwenye malezo na makuzi ya watoto wao.


“Kila Mzazi aone kuwa analo jukumu la malezi na makuzi ya mtoto wake. Hiki alichokifanya Mhe. Rais ni kuunga mkono juhudi kubwa ambayo mnaifanya kwa hayo makundi ambayo mnayahudumia lakini pia ni faraja kuwa anatambua na kuthamini kazi kubwa ambayo mnaifanya” Mhe. Senyamule


Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri amesema, jambo alilolifanya Mhe. Rais ni sadaka ambayo sisi tunatakiwa kuiga ili kuweza kufanikiwa katika mahitaji yetu binafsi kwani pale tunapotoa kwa wengine ndipo tutapata zaidi.


Akiainisha mahitaji yaliyotolewa na Mhe. Rais, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya amesema;


“Dodoma ni moja kati ya Mkoa ambao Mhe. Dkt. Samia anaendeela kutukumbuka na kutupenda katika nafasi tofauti tofauti. Zawadi tulizopokea ni magodoro 477, Mashuka pea 450, Mablanketi 500, kilo za Sukari 1000, Maharage kilo 600, Mafuta ya kupikia dumu 13 za lita 20 kila moja, Unga wa Ngano kila kiroba kina kilo 25 na hapa tuna viroba 52 na Mchele kilo 2000”


Nae, Mwakilishi wa Vituo vilivyokabidhiwa msaada huo kutoka kituo cha watoto yatima cha Alhaafidh Islamic Centre, Wilaya ya Kondoa, Hajat Aisha Nobbe amemshukuru Mhe. Rais Samia na kusema kuwa wanamuombea dua kila wakati na huo umekua ni utaratibu wa kawaida kila wanapokutana kwa ajili ya ibada.


Msaada huo kutoka kwa Mhe. Rais Dkt. Samia, umekabidhiwa kwa wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dodoma ambapo utakwenda kugawiwa kwenye vituo 13 ambavyo vimekusudiwa na kutumika kusaidia watoto pamoja na watu wenye mahitaji maalumu ili kupunguza mzigo kwa watoa huduma wa vituo hivyo.




#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.