• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RAS GUGU AKUTANA NA WADAU WA KOFFIH

Imetumwa : August 30th, 2023

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu amefungua kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mradi ya uboreshaji wa huduma za afya ya uzazi na mtoto kwa Halmashauri ya Mpwapwa kilichofanyika leo tarehe 30 agosti 2023 katika ukumbi wa Hospitali ya Mpwapwa.

Akizungumza katika kikao hicho Gugu amesema ni vyema kuzingatia mikakati iliyopo ili miradi ambayo ipo katika Halmashauri inakamilika kwa wakati na kuleta manufaa kwa wananchi.

Amesema wataalamu wanatakiwa kuhakikisha miradi inatekelezwa na kusimamia kwa ubora kama serikali ilivyokubaliana na wadau wa KOFIH kwa lengo la kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati kama ilivyokubalika.

“Kila Halmashauri ni lazima kuhakikisha vifaa tiba vinanunuliwa kwa wakati na wananchi  waweze kuvitumia, kunufaika na kuongeza tija kwa wananchi.

“Serikali yetu inatoa kipaumbele kwenye suala la afya hivyo tunaona Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa kipaumbele kwenye suala la afya ya mama na mtoto hivyo ni lazima tuhakikishe miradi yetu tunaipa kipaumbele” amesema Gugu


Naye Katibu  Tawala Msaidizi,  Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dodoma Dkt. Best Magoma amesema kikao hicho kina lengo la kuhakikisha miradi ya KOFIH inatekelezwa kwa wakati na kuweka mikakati ya ukamilishaji wake.

“Miradi inakuja ili wananchi waweze kupata huduma kwa ukaribu na kuweza kuokoa na kupunguza changamoto za wananchi”


Kwa upande wake Katibu wa afya Bi. Nice Moshi ameipongeza Halmashauri ya Mpwapwa kwa kujitokeza kwa wingi kuunga mkono  jitihada zinazotolewa na kuletwa na wadau wa KOFIH katika Halmashauri ya Mpwapwa

“KOFIH imeleta miradi ya afya na vifaa  tiba kwa ajili ya wananchi wa wilaya ya Mpwapwa hivo pongezi kwa KOFIH na kuna baadhi ya hospitali zilizofadhiliwa  zimeshaanza kutoa huduma za afya ambazo zimejengwa kwa fedha za KOFIH ambapo mwanzoni wananchi hao walikuwa wanafuata huduma hiyo mbali na hospitali ya Wilaya na kuweza kupata mafunzo kwa watumishi”.amesema Mosha.

Kikao hicho ni cha Pili ambapo kikao cha kwanza kilifanyika tarehe 15 Juni 2023 katika Halmashauri ya Mpwapwa.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.