• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC DKT. MAHENGE AKUTANA NA MWENYEKITI BODI YA KOROSHO MAMA ANNA ABBDALLAH WAZUNGUMZIA KUKUZA KILIMO CHA ZAO HILO KWENYE MKOA WA DODOMA

Imetumwa : May 14th, 2018

RC DKT. MAHENGE AKUTANA NA MWENYEKITI BODI YA KOROSHO MAMA ANNA ABBDALLAH WAZUNGUMZIA KUKUZA KILIMO CHA ZAO HILO KWENYE MKOA WA DODOMA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge leo Mei 14, 2018 amekutana na Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania Mama Anna Abdallah na kufanya nae mazungungumzo juu ya kukuza kilimo cha zao la Korosho kwenye Mkoa wa Dodoma.

Katika mazungumzo yao Dkt. Mahenge amemjulisha mama Anna Abdallah kuwa wakulima wa maeneo mbalimbali ya Halmashauri za Mkoa wa Dodoma wameitikia kwa kasi kilimo cha zao la korosho linalofanya vizuri kwenye soko kwa sasa. Amesema Msimu uliopita Bodi iliupatia Mkoa wa Dodoma zaidi ya kilo 9000 za mbegu za Mikorosho lakini hazikutosheleza mahitaji hivyo ameomba Bodi kuongeza zaidi mbegu kwenye Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kuzipanda wakati wa msimu mpya wa kilimo.

Dkt. Mahenge pia ameiomba Bodi ya Korosho kuangalia uwezekano wa kuwalipa wakulima/wadau/Taasisi zilizotumika kuandaa na kuhudumia vitalu vya kuotesha miche ya Mikorosho na kisha kuisambaza na kuigawa kwa wakulima ili kuwawezesha Wadau hao kuendelea kuandaa miche mingi zaidi ya mikorosho na kuigawa kwa wakulima ili kuhakikisha kilimo cha zao hilo linalofanya vizuri kwenye soko kinakua hapa Mkoani Dodoma.

Amesema mwamko wa wakulima wa Mkoa wa Dodoma juu ya zao la Korosho ni mkubwa na Tafiti iliyofanywa na wataalamu wa kituo cha utafiti wa kilimo cha Naliendele imeonesha kuwa Ardhi na Hali ya Hewa ya Mkoa wa Dodoma inauwezo mkubwa wa kustawisha zao la Korosho.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania mama Anna Abdallah amemhakikishia Dkt Mahenge Kuwa Bodi ya Korosho itasaidia jitihada za Mkoa wa Dodoma za kukuza Kilimo cha zao la Korosho ambalo limeungwa mkono kwa nguvu kubwa na Wakulima wa Halmashauri za Wilaya za Mkoa wa Dodoma.

Mama Anna Abdallah amemjulisha Dkt. Mahenge kuwa Bodi imetenga kiasi cha Tani 300 za mbolea aina ya Sulphur Kwa ajili ya kuzigawa kwenye maeneo Mapya yaliyoanzisha Kilimo cha Korosho ikiwemo Mkoa wa Dodoma. Aidha, ameahidi kutembelea wakulima wa korosho kwenye halmashauri za wilaya za Kongwa, Mpwapwa, Bahi, Chamwino na kondoa ili kujionea hali ya kilimo cha korosho kwa wakulima waliotangulia kuitikia kilimo cha zao hilo Mkoani Dodoma.


Mwenyekiti huyo wa Bodi ya Korosho mama Anna Abdallah kupitia kwa Mkuu wa Mkoa Dkt. Binilith Mahenge, amewatoa hofu wakulima/wadau/Taasisi zilizohusika kuandaa na kuhudumia vitalu vya kuotesha miche ya korosho ili kuigawa kwa wakulima kuwa baada ya mchakato wa bajeti unaoendelea hivi sasa kwenye bunge la bajeti, wanatarajia Serikali itatenga fedha za kuwalipa kwa kazi hiyo waliyoifanya na kuwataka wawe na subira.

#OFISIYAMKUUWAMKOADODOMA

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.