• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC SENYAMULE AKAGUA UJENZI WA MADARASA SHULE ZA SEKONDARI DODOMA JIJI

Imetumwa : November 10th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amefanya ziara ya kukagua ujenzi unaoendelea wa madarasa ya shule za sekondari za Dodoma Jiji, madarasa yanayojengwa kwa fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya kukidhi nafasi kwa wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2023.

 Mkoa wa Dododma umepokea kiasi cha Tsh.6,780,000,000/- kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 339, katika shule 127, zilizopo katika halmashauri 8 za Mkoa huo.

Miongoni mwa shule ambazo mkuu wa mkoa ametembelea katika ziara  hiyo ni shule ya sekondari Viwandani na shule ya sekondari Zuzu. Shule hizi zote zinaendelea na ujenzi wa vyumba vya madarasa ambapo kila moja inajenga madarasa mawil. Madarasa hayo yamefikia hatua ya kuezeka na kumalizia hatua za mwisho.

Akiwa shule ya sekondari Zuzu, Mkuu wa Mkoa amewataka wasimamizi wa ujenzi wa mradi huo kusimamia mradi huo ili umalizike kwa wakati.

“Hakikisheni mnamaliza lakini kwa uzuri, ubora na uharaka, hakikisheni mnamalizi mradi kwa wakati. Rais ametoa fedha shilingi Bilioni 6.780 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 339 kwenye shule mbalimbali za mkoa wa Dodoma. Tuna jukumu la kusimamia fedha hizi zitumike ipasavyo” RC Senyamule

Akitoa taarifa ya ujenzi huo mbele ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa shule hiyo Bw. Hezron Lupondo, amesema shule ilipokea shilingi Milioni 20 kwenye akaunti ya shule kwa ajili ya ujenzi wa madarasa hayo.

“Mradi ulianza Oktoba 10 na mpaka sasa umefikia hatua ya upauaji, kuweka kenchi, plasta, madirisha na milango. Tunatarajia mpaka Novemba 20 mradi utakua umekamilika” Amesema Bw. Lupondo

Mbali na ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa ametoa rambirambi za Serikali ya Mkoa kwa Familia ya Marehemu Neema Faraja Samwel ambaye alikua mwenyeji wa Dodoma na mfanyakazi wa Shirika la MDH, aliyepoteza maisha kwenye ajali ya ndege iliyotokea mkoani Kagera Novemba 6.

" Natoa pole kwa familia ya Neema, mshikeni sana Mungu wakati huu pia natoa pole kwa Shirika la MDH kwa kupoteza wenzao kwani tunajua shirika hili linafanya kazi kwa karibu na Serikali. Serikali imeshiriki msiba huu kuanzia Kagera tulipowakilishwa na Mhe. Waziri Mkuu. Serikali imeguswa sana kwani ni tukio lililotushtua  na Serikali inaendelea kuchunguza chanzo cha ajali. Serikali ya Mkoa inatoa rambirambi ya Shilingi Milioni moja na tunaahidi kuendelea kushirikiana kwa karibu na familia katika kila hatua” Amesema Mhe. Senyamule

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.