• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC SENYAMULE AMTAKA MKANDARASI WA UCHIMBAJI WA VISIMA VYA UMWAGILIAJI KUKAMILISHA MRADI KWA WAKATI

Imetumwa : February 6th, 2025

Na. Francisca Mselemu

      Habari - Dodoma RS


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule amemtaka Mkandarasi wa kuchimba visima vya umwagiliaji katika Mkoa huu, kuhakikisha kuwa  anakamilisha mradi huo kwa wakati ili wakulima waweze kunufaika na uwekezaji ambao ni muendelezo wa jitihada za Serikali ya Daktari Samia Suluhu Hassan  kukuza sekta ya kilimo pamoja na kuwainua Wakulima Kiuchumi.

Mhe. Senyamule ameyasema hayo  wakati wa hafla ya  makabidhiano ya eneo kwa ajili ya uchimbaji wa kisima cha umwagiliaji liyofanyika katika Mtaa wa Chamwino kata ya Chihanga, Jijiini Dodoma.

"Tumeambiwa mradi huu utachukua miezi sita (6) tu, leo ni mwezi wa pili, mwezi wa Nane (8) mradi huu unatakiwa uwe umekamilika. Sisi mradi huu ni kati ya vipaumbele vya Mkoa wa Dodoma, tungetamani mradi huu ujengwe kwa wakati, tungetamani mradi huu uishe kwa muda uliokusudiwa. Nimeambiwa hili hapa ni soko. Mradi ukamilike, hili soko lianze kupata bidhaa nyingi, kwa sababu ni kubwa, magari yawe yanapaki hapa.

"Na bahati nzuri, wewe ndio umepewa mradi huu mkoa mzima, tunasema Dodoma ni fahari ya Watanzania, sisi tunataka uifaharishe Dodoma. Miradi ya Elimu, miradi ya Afya, Dodoma tumepata tuzo kwa kufanya vizuri. Sasa hatutamani mradi huu wanakuja kusema wapi pamekamilika, Dodoma hakujakamiika.'' Amesisitiza Mhe. Senyamule.

Akimkaribisha  Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Bw. Kaspar Mmuya amewasisitiza Wananchi kuwa kaulimbiu ya Mkoa  ya mwaka 2025 ni Umasikini sasa Basi, na kwamba kaulimbiu hiyo inatekelezwa kwa vitendo kwa kuhakikisha Wananchi wa Dodoma ambao wengi wao  ni wakulima, wanalima kilimo cha uhakika na chenye tija.

Naye  Meneja wa Umwagiliaji mkoa wa Dodoma, Mhandisi Oswald Urassa, amesema mradi huo ni utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais ambapo unatarajiwa kunufaisha wakulima 27,600 nchi nzima, huku  kila Halmashauri ikitarajiwa kupata visima kumi(10). Katika awamu ya kwanza vitachimbwa visima sabini(70), Mkoa wa Dodoma utapata visima sita (6) ambavyo vitachimbwa katika wilaya za Kondoa, Bahi, Kongwa, Chemba, Chamwino na Dodoma.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Chihanga amemshukuru sana Mhe. Rais kwa mradi huo, ambao amesema kwamba  utamfanya apate usingizi kwani siku zote amekuwa akiwaza  kuhusu Wananchi  wa kata yake wanaojishughulisha na kilimo cha umwagiliaji  mbao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa maji kutokana na kisima wanachokitegemea  ndicho kinachotumika kwa matumizi mengine ya kibinadamu ya wakazi wa eneo hilo.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.