• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC SENYAMULE ASIKILIZA KERO ZA MADIWANI,WATUMISHI NA WANANCHI WA DODOMA JIJI

Imetumwa : October 20th, 2022


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amefanya kikao na kuongea na watumishi wa Halmashauri ya Dodoma Jiji katika ukumbi wa Halmashauri hiyo uliopo katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.

Dhima ya mfululizo wa vikao hivi na watumishi wa Halmashauri za Mkoa wa Dodoma ni kusikiliza kero za watumishi na kuzipatia majawabu kutoka kwa wataalamu wa idar mbalimbali za Mkoa ambao ameambatana nao Pamoja na kutoa maagizo ya Serikali kuu yanayotolewa kwa waandishi.

Baada ya watumishi wakiwemo madiwani kuwasilisha kero kadha wa kadha ikiwemo changamoto za maji, umeme, barabara, migogoro ya ardhi nk. Wakuu wa idara wamezipatia majawabu na nyingine Mhe. Senyamule mwenyewe amezijibu na baadhi kuahidi kuzibeba na kwenda kuzifanyia kazi.

Akitoa maagizo yake pamoja na yale ya Serikali Kuu, Mkuu wa Mkoa amegusia zaidi suala la elimu ambalo hugusa kwenye kila Halmashauri anayotembelea. Amesema Halmashauri ya Dodoma peke eina upingufu wa vyumba vya madarasa 1700 ambapo amewataka kujidhatiti kumaliza tatizo hili kwani Serikalai Kuu peke nyake haiwezi kulimaliza kwa wakati.

“Tujifunge mkanda, tuweke mpango wa kumaliza tatizo hili kwani tukiweka mkakati kwa wananchi kushiriki kuchangia na Serikali ikimalizia basi tatizo litakwisha. Watendaji wa vijiji mumejisahau kushiriki suala la miundombinu ya Elimu, wananchi wapo tayari kushiriki lakini hamuwashirikishi”

“Kakaeni vikao mkashauriane nama ya kupunguza tatizo la changamoto ya miundombinu ya elimu kwani Jiji wamepewa fedha za ujenzi wa madarasa 29 tu wakati uhitaji wao ni madarasa 1700, kwa kuiachia Serikali tu tatizo hili halitakwisha. Tushirikiane na wananchi ili tuongeze ufaulu kwa wanafunzi wetu kwani kiujumla Dodoma hatufanyi vizuri” Amesisitiza

Jambo jingine aliloligusia kwa upana ni masuala ya ardhi. Mhe. Senyamule ameonyehwa kukerwa na usumbufu wanaoupata wananchi pale wanapouziwa maeneo ambayo tayari yana majina ya wamiliki wengine (Double allocation)

“Zichukuliwe hatua kwa wanaofanya double allocation, Jiji tunatakiwa kuongeza utashi kwenye utatuzi wa migogoro ya ardhi kwani kuwepo kwetu Dodoma ni kwa lengo la kutatua kero za ardhi. Tufanye, mabadiliko ya mfumo ambao unachelewesha kupata huduma kwa wananchi” RC Senyamule.

Pia Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amefanya mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Mtumba kusikiliza kero zinazowakabili pamoja na kuzipatia majawabu ambapo baadhi ya kero zilizowasilishwa mbele yake ni pamoja na migogoro ya ardhi, ugawaji viwanja, maji, nauli ya usafiri kwenda Dodoma Mjini, barabara za mitaa, miundombinu ya shule za msingi n.k

Mhe. Senyamule amewataka wataalamu wa idara mbalimbali ambao kero za wananchi hao zimewagusa, kuzijibu kisha yeye atamalizia kwa msisitizo. Wataalamu wa maji, ardhi, pamoja Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma wamejibu kero hizo.

Baada ya wananchi kupata majibu ya changamoto zao, Mhe Mkuu wa Mkoa ameongea na wananchi wa Mtumba kukazia majibu hayo na amegusia suala la ulinzi na usalama ambalo liliwasilishwa kwake kuwa ni kero.

“Suala la ulinzi na usalama wa wananchi ni kipaumbele cha Serikali. Tuna tangaza kiama kwa wabakaji wote wa wanawake kwenye Kata hii kwani hatuwezi kuvumilia suala hili. Naagiza RPC ushughulikie hili”

Aidha Mkuu wa Mkoa amesema kuwa Mtumba ni eneo la kimkakati kwa maendeleo ya Dodoma na ameahidi kutoa ushirikiano wake kupitia ofisi ya Mkoa kwani amejiwekea utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi kila siku ya Jumatano ya wiki pia ametaja namba ya simu ya bure ambayo mwananchi yeyote mwenye kero anaweza kutuma ujumbe wa bure ambayo ni 0800110083.

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.