• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Rc SENYAMULE , Asikiliza Kero za Wananchi wa Kongwa

Imetumwa : September 1st, 2022

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Staki Senyamula hivi karibuni  amefanya ziara Wilayani Kongwa na kusikiliza kero za wananchi wa wilaya ya Kongwa.

Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa alipata fursa ya kuongea wa wanakijiji wa kata ya Mkoka kijiji cha  Songamble A na Songambele B. Akizungumza Kuhusu kijiji Cha Songambele ,Diwani wa kata ya Mkoka, Mhe. Richard. F. Mwite, amemweleza mkuu wa mkoa kuwa kata ya Mkoka ni kati ya kata 22 Za Halmashauri hiyo na  ina vijiji viwili, kijiji cha  Songambele A na  Songambele B.Pamoja na kupokea fedha kwa ajili ya mradi wa maji na mradi wa kikuo cha afya baadhi ya vijiji katika eneo hilo bado havina umeme wala maji.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa hizo,Mkuu wa Mkoa wa Dopdoma Mhe. Rosemary Senyamule aliwaeleza wananchi wa Songambele kuwa kati ya kata 130 za mkoa wa Dodoma kata ya Mkoka ni kata ya kwanza kutembelewa na Mkuu wa Mkoa. “ Ziara yangu ina agenda tatu tu  kwanza kujitambulisha kwenu,pili kusikiliza kero na tatu  kutoa maelekezo ya Serikali’’ Amesema RC- Senyamule. Kabla ya kuongeza siku za Sensa, tayari mkoa wa Dodoma ulikuwa umefikia106%, hongereni sana. Pia niwapongeze sana kwa kuupokea mwenge wa uhuru ambapo miradi yoye ya Wilaya ya Kongwa ilipita  hongereni na ahsanteni kwa ushirikiano.

Baada ya Kusema hayo Mkuu wa Mkoa alitoa fursa kwa wananchi wa Songambele A & B kuwasilisha kero zao ambapo jumla ya watu 11 waliuliza maswali na kuwasilisha kero zaidi 20, ambazo zilihusisha masuala binafsi na maendeleo ya Wilaya, kutia ndani huduma za afya, barabara, vivuko, matumizi ya mapato kutokusomwa kwa kipindi cha mwaka miaka mitatu.Ubadhilifu wa fedha za mradi wa Songambele A & B,kiwanja cha mpira kilichopo eneo la wazi /open place , kimebadillishwa matumizi na  kuwa Bonde kwa kipindi cha  miaka 3,wanafunzi wa kike  kuwekwa kinyumba ombi kujengwe hostel,watu hawathamini mazingira.Shule ya Isanga haina maji na vyoo vinavyotumia maji.Miradi ya vijana ifikie Songambele,vijana wapate mradi utakaowaongezea kipato.Elimu rika itolewe Kwa vijana na kijana aliyeomba pampu ya maji ili aweze kuendeleza kilimo cha mboga

Aidha Mkuu wa Mkoa aliwaalika watalam kutoka kila idara ambayo ilielekezewa kero kujibu hoja za wananchi.Aidha baada ya majibu kutoka kwa viongozi hao Mkuu wa Mkoa amempa  mtendaji wa kijiji wiki mbili kushughulikia tatizo la usomaji wa taarifa ya mapato Na matumizi  na kuhakikisha taarifa inasomwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu.

Mhe.Senyamule amewata Viongozi wote wa Wilaya ya Kongwa  kutenga  nafasi ya kusikiliza kero za Wananchi na kutoa taarifa kila mwenzi.Kero nyingi ziwe zinapata ufumbuzi.Lengo la Mhe. Rais ni kuhakikisha kuwa ifikapo Dec, 2022 vijiji vyote Tanzania viwe vimewashwa umeme, hivyo mkoa wa Dodoma tukiwa Makao makuu tunapaswa kuwa mfano katika hili.

Aidha Mkuu wa Mkoa amewataka wananchi kutoa taarifa za kweli na sahihi wanapojiandikisha kwenye masuala ya ruzuku na kutumia majina yanayopatuka aidha kwenye vitambulisho vyao vya NIDA au vya kupigia kura .Kumekuwa na tabia ya  baadhi ya wafugaji kuwapa fedha  viongozi na hivyo kuwa rushwa na kuwapotezea muda wananchi kwa kuchelewesha maamuzi yanapohusu migogoro ya ardhi. Mkuu wa mkoa aliahidi kumnunulia pump kijana aliyeomba msaada huo.

Mhe. Senyamule  ametaja vipaumbele vya Mkoa ikiwa ni pamoja na  utunzaji wa mazingira, Sekta ya Kilimo, kwani asilimia kubwa ya wananchi wa Kongwa wanategemea Kilimo, maafisa ugani wamepewa pikipiki na bodaboda. Serikali itatoa mbolea kwa ruzuku ,Serikali imabwawa ya umwagiliaji, kwani mvua haitabiriki.Hivyo,Halmashauri zote zimeelekezwa zitafute maeneo ambayo wananchi wataweza kulima Kwa pamoja. Tuna mabwawa mawili mkoa wa Dodoma Chamwino na Mpwapwa.

Mkuu wa Mkoa amewaagiza wananchi wa Songambele A & B kuzingatia masuala matatu muhimu ambayo ni, mosi, Chanjo ya polio, pili, Mkulima asiache kuandikishwa kwa ajili ya mbolea ya ruzuku, jina liwe sahihi na liwe lile ambalo anatumia kwenye litambulisho cha NIDA au cha mpiga kura.Tatu,suala la Mifugo kuvalishwa hereni.Aidha Mkuu wa Mkoa amewafahamisha wanasongambele kuwa kauli mbiu ya mkoa wa Dodoma ni “Dodoma Fahari ya Watanzania”.

Aidha mkuu wa mkoa ametia Shime kwenye Elimu, tusiwe vuguvugu bali tuwe moto ili kuongeza ufaulu wa watoto wetu.Wazazi, Shule ya Msingi, Kijiji, Shule ya Sekondari, O- level kata,tuwe na mkakati na tuwape kazi wakandarasi  ili tupunze changamoto ya madarasa.Tuendelee kujenga madarasa.Mkuu wa Mkoa aliwapa wananchi namba ya simu ya kupiga endapo watakabiliana na changamoto  yeyote namba hiyo ni 0800110083.

Nae Katibu Tawala Mkoa  wa Dodoma Dkt. Fatuma Mganga, amewasisitiza  wakazi wa Songambele A & B kujiunga na Bima ya Afya kwani majanga ya afya hayapigi hodi,. Dkt. Mganga amesema  6% tu ya kaya zote za mkoa wa Dodoma  ndizo zenye Bima ya afya.“Anzisheni utaratibu wa wale walikata Bima wahudumiwe kama mfalme. Katika kila kituo pawe na namba ya simu  ya mganga mkuu, na kama hakuna Dawa. apigiwe  simu mganga Mkuu na alezwe hilo.Watumishi wa afya,tufanye  kazi kama wataalamu kwani dawa ya kumtibu mgonjwa haipo moja tu ikikosekana moja basi apewe nyingine.Kila asubuhi fanyeni  vikao vya asubuhi (morning breakfast) na mjue ofisi yenu ina Dawa gani.Wataalam twende tukabadilike.Mganga Mkuu hakikisha tunabadilika.Wananchi hawa ndio waajiri wetu”.Amesisitiza Dkt. Fatuma Mganga.Mwisho

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.