• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC SENYAMULE ATAKA MABADILIKO IDARA YA ARDHI DODOMA

Imetumwa : October 15th, 2022


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ameitisha kikao na watumishi wa Idara ya ardhi Mkoa wa Dodoma kwenye ukumbi wa Ofisi yake uliopo kwenye jengo la Mkapa, Barabara ya 8 ili kujadili migogoro mbalimbali ya ardhi inayoukabili Mkoa na kutafuta suluhu yake.

Kikao hicho kiwewahusisha watumishi wa idara ya ardhi, wakurugenzi wa Halmashauri zote 8 za Mkoa ambao ndio wamehusika kusemea changamoto za ardhi zinazozikabili halmashauri zao.

Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Dodoma Bw. Thadei Kabonga amefungua kikao hicho kwa kuchanganua aina mbalimbali za migogoro iliyopo katika idara ya ardhi, changamoto zake na namna ya kuitatua.

“Ni lazima Maafisa ardhi wote tujue tunahusika na changamoto hii na baadhi ya tatuzi zake ni kufungua barabara kwenye maeneo yaliyopimwa ili kurahisisha kufikika kwa urahisi pia kuna baadhi ya Taasisi za umma zinachukua maeneo ya wanachi wakati hawana uwezo wa kuwalipa fidia. Hapa msimamo wa Wizara ni kuzitaka taasisi zisichukue maeneo ya watu kama haziwezi kulipa fidia kwani zinazalisha migogoro kwa wanachi” Amesema Bw. Kabonga

Nao wakurugenzi wa Halmashauri wamewasilisha kero za ardhi zinazowakabili ikiwa ni pamoja na ukosefu wa vitendea kazi kama vifaa vya kupimia ardhi, usafiri, upungufu wa watumishi kwenye idara, ukiukwaji wa sheria za ardhi kwenye idara pamoja na baadhi ya watumishi wasio waadilifu kushirikiana na wananchi kuzalisha migogoro

Mkuu wa Mkoa akizungumza na watumishi hao baada ya kusikiliza kero zilizowasilishwa ambazo zilipatiwa majawabu kutoka kwa Kamishna wa ardhi pamoja na Mhe. RC. Amesema kuwa watumishi wanapaswa kuwa na utaratibu wa pamoja wa kutatua migogoro ya ardhi kwani ni muhimu sana katika kuitatua kwa wakati.

“Tusiikimbie migogoro bali tuimalize kwani ndio kazi yetu. Nataka tujipe muda hadi mwezi Desemba mwaka huu migogoro yote inayoweza kutatulika itatuliwe. Kaimalizeni hiyo migogoro, tukiamua kuimaliza hii migogoro kwa Dodoma inawezekana, tukakae vikao tuamue hilo” RC Senyamule

Kadhalika, Mhe. Senyamule ametoa rai kwa watumishi hao kuwa wamepewa dhamana ya kutunza kitu kisichoongezeka na kuwataka kufanya kazi kwa uadilifu na heshima kubwa

“Rais anataka haki itendeke lakini sisi watumishi wake hatufanyi haki, mumepewa dhamana ya ardhi, nendeni mukatusaidie kuwapa haki wale waliokoseshwa haki zao kwa ukweli tuwasaidie” Ameongeza.

Hata hivyo, ameendelea kusisitiza kuwa watumishi wa ardhi wamepewa dhamana ya kutengeneza taswira ya nchi kupitia Dodoma hivyo wanapaswa kulinda kauli za viongozi wa nchi wanapokua nje ya nchi na kutoa sifa kwa nchi yetu kwani wanafanya kazi kubwa kuitangaza sifa ya nchi kimataifa na kuvutia wawekezaji.

“Natamani kuona mabadiliko makubwa kwenye idara ya ardhi nawaomba mukabadilike” Amesisitiza

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.