• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC SENYAMULE ATATUA MGOGORO WA UJENZI WA SHULE KIDOKA - CHEMBA

Imetumwa : October 31st, 2024

Na. Hellen M. Minja,        

       Habari – DODOMA RS

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule, leo Oktoba 31, 2024, ametatua mgogoro kati ya wananchi wa Kata ya Kidoka juu ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kata, kufuatia Wananchi wa  vijiji viwili vya Kidoka na Pangalua  vilivyoko katika kata ya Kidoka,Halmashauri ya wilaya ya Chemba, wote kutaka   shule ijengwe kwenye vijiji vyao.

Mkuu wa Mkoa huyo ametatua mgogoro huo wakati wa mkutano wa hadhara kwenye Kijiji cha Pangalua,mkutano ambao lengo lake ni  kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili wakazi wa kata hiyo,ikiwemo eneo la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata.

“Serikali imeona wote mna mahitaji ya shule, mabishano haya yanatokana na dhamira njema, japo inatuchelewesha kwani ilitakiwa kufanyiwa maamuzi ya haraka. Tumeamua shule zijengwe mbili, kwa maana ya Kidoka na Pangalua. Shule mbili zitajengwa, kila Kijiji  kipate ya kwake” Amesema Mhe. Senyamule.

Baada ya uamuzi huo, Mkuu wa Mkoa amesema fedha zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa shule moja, sasa zitagawanywa kwa ujenzi wa shule mbili na kuwaasa wazazi kupeleka watoto wao shule.

“Hizo fedha zitagawanywa mara mbili, Kidoka itakwenda shilingi 249,763,750 na Pangalua itakuja shilingi 294,461,876. Nimesikitika kwa kuwa leo nilijipanga kuja kuanza ujenzi maana tumechelewa miezi minne nyuma, tuna miezi miwili tu kukamilisha haya majengo ili mwezi wa kwanza, watoto wetu waanze shule”. RC Senyamule

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe. Halima Okash, amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kumaliza mgogoro huo kwani wananchi wa Kata hiyo sasa watakua na amani.

“Hapa najua wanachi hawa wakiondoka, nafsi zao zitakua zimetulia sana kwa sababu mgogoro huu wa ujenzi wa shule umetatatuliwa. Mhe. Mkuu wa Mkoa tunakushukuru sana. Sisi kama Serikali katika ngazi hii ya Wilaya, Tarafa, Kata pamoja na Kijiji,tumepokea maelekezo yako na tupo tayari kuyatekeleza” DC Okash.


#kurayakosautiyako              

#ujanjanikupigakura              

#dodomatukotayarikupigakura

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.