• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC SENYAMULE ATEMBELEA, AFANYA UKAGUZI SOKO JIPYA LA MACHINGA

Imetumwa : November 3rd, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyemule ametembelea na kufanya ukaguzi katika mitaa iliyokua ikitumiwa na wafanya biashara ndogondogo maarufu kama machinga wa Jiji la Dodoma ambao kwa sasa wamehamia kwenye eneo maalumu walilotengewa kwa ajili ya biashara zao lililopo Bahi road.

Mhe. Senyamule amekagua maeneo ya Independence squre, oneway na Nyerere squre ambayo yote kwa sasa yamepata mwonekano mpya baada ya vibanda vyote kubomolewa, maeneo kusafishwa na kubaki wazi

“Nawashukuru sana machinga kwa kukubali kuhamia hapa kwani sasa mitaa ya Jiji letu imepata sura mpya mfano pale oneway, unaweza kusimama independence squre ukaweza kuona mpaka mwisho wa barabara. Kwa kweli nawapongeza sana” RC Senyamule

Vile vile, Mhe. Senyamule amefurahi kuona wafanyabiashara hao wanafanya kazi kwa amani bila shida yoyote na mwonekano wa soko sasa umekua bora zaidi na pia ametoa maagizo kwa Halmashauri ya Jiji.

“Nafurahi leo tumetembelea hapa kukiwa na wauzaji maana kipindi chote ilikua ni kuja kutoa maagizo tu lakini sasa panaonekana kwa sura mpya. Nitoe maagizo kwa Jiji kuchukua hatua za haraka za kusafisha mitaa yote iliyokuwa ikitumika awali. Pia kwa soko hili, tuendelee kutunza mazingira, kamati za mazingira tukumbushane suala la usafi ili mahali hapa pawe na mandhari nzuri” Amesisitiza

Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jiji Mhe. Jabir Shekimweri aliyeambatana na Mkuu wa Mkoa katika ukaguzi huo, amesema ;

“Mpaka sasa machinga kwa umoja wao ambao tayari wameshahamia hapa ni asilimia 95. Jana tulipita kufanya ukaguzi kwenye mitaa kama tulivyofanya leo ili kuhakikisha hakuna machinga anayebaki mitaani na tunafanyia kazi maelekezo yako yote Mhe. Mkuu wa Mkoa, ikiwa ni p amoja na kuharakisha kuanza kwa kituo cha daladala hapa, usalama wa eneo hasa kwa upande wa kivuko kwenye barabara kubwa, tayari tumeweka alama za zebra na pia tumepata ushauri wa kuweka taa za barabarani” DC Shekimweri

Serikali ya Mkoa imeahidi kutoa ushirikiano wa karibu kwa wafanyabiashara hao kwa kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha machinga wanapata maeneo maalum ya kufanyia biashara zao kwani kwa Dodoma zimetimia na kuwataka wafanya biashara hao kulifanya eneo hilo kuwa la kitalii kwa kuwa na mwonekano wake wa kuvutia kama linavyoonekana hivi sasa.

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.