• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC SENYAMULE AWAHIMIZA WANAWAKE WAJAWAZITO KUZINGATIA MAELEKEZO YA WAHUDUMU WA AFYA

Imetumwa : November 17th, 2024

Na;Happiness E. Chindiye

     Habari - Dodoma RS

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule amewahimiza wanawake wa Mkoa  huu na kote Nchini, kuzingatia maelekezo wanayopatiwa na Madaktari kipindi wanapogundua kuwa na ujauzito kwa kuhudhuria kliniki ili kusaidia kuimarisha usalama wa mtoto wakati wa kujifungua.

Wito huo umetolewa wakati wa Maadhimisho ya siku ya Mtoto  Njiti Duniani  ambayo hufanyika Novemba 17 kila mwaka, ikiwa ni  kutambua thamani ya uhai wa Mtoto aliyezaliwa mapema sana (Watoto Njiti) na kuondokana na  imani potofu kuwa Watoto wa aina hiyo ni laana au mkosi.

Maadhimisho hayo yamefanyika Kimkoa kwenye viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ambapo Mhe. Senyamule amesema,

"Nawasihii Wananchi wa Mkoa wa Dodoma zingatieni  maelekezo mnayopewa  na Madaktari pindi mnapogundua  kuwa na  ujauzito kwa kuwahi kuhudhuria kliniki mapema ili kupunguza athari zinazoweza kuepukika” .

Mhe. Senyamule ameongeza kwa kutoa wito kwa Wahudumu wa Afya kuendelea kufanya kazi kwa weledi  ili kunusuru kizazi hicho.

Naye Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa  Dodoma  Dkt.Baraka Mponda amesema Hospitali ya Rufaa Mkoa  Dodoma imeendelea kupunguza Vifo vya Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati  (Njiti) ambapo kati ya watoto elfu moja, kumi na mbili pekee ndio waliofariki kutokana na sababu mbalimbali za kiafya ikiwemo mama Wajawazito kutohudhuria Kliniki mapema.

Dkt. Mponda amesema mafanikio hayo yametokana na uboreshaji wa huduma  ikiwemo huduma ya  Kangaroo, mashine za joto, kliniki na utoaji wa elimu  kuhusu malezi ya watoto hao.

Maadhimisho hayo yameongozwa na kauli mbiu isemayo “ Zaidi ya watoto Milioni 13 huzaliwa mapema sana kila mwaka. Upatikanaji wa huduma bora kwa kila mtoto unahitajika kila mahali alipo” . Huku takwimu zinaonesha kuwa kati ya watoto 2500 wanaozaliwa hospitalini hapo, watoto 1000 huzaliwa wakiwa njiti.


&&&


#kurayakosautiyako  

#ujanjanikupigakura                #dodomatukotayarikupigakura

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.