• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC SENYAMULE AZINDUA WARSHA YA MAKASISI KANISA LA ANGLIKANA KANDA YA KATI

Imetumwa : October 12th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amezindua Warsha maalumu ya Makasisi wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika ambapo amealikwa kama mgeni rasmi.

Warsha hiyo imelenga  kuzungumzia mahusiano ya uchumi na Kanisa kwani Kanisa hilo limejikita katika shughuli mbalimbali za kiuchumi kama vile Kilimo, uwekezaji katika majengo bora na  utunzaji wa mazingira.

Mhe. Senyamule amelipongeza Kanisa hilo kwa kushiriki katika kuinua uchumi kwani ndilo jambo ambalo Serikali inashughulika nalo kila uchao. “Nawapongeza sana kwa kuwekeza kwenye uchumi kwani tunatakiwa kurithi utajiri wa uchumi wa Kanisa. Hata kwenye maandiko matakatifu Mfalme Suleiman aliweza kujenga hekalu kubwa lenye mawe ya thamani kama dhahabu  na kadhalika kwa sababu alikuwa na uchumi mzuri na mkubwa”.

“Ukizungumza na watu , baadhi ya watu  wamekuwa wakiniambia hali ya hewa ya Dodoma inafanana na hali ya hewa ya  Israel, nasi basi turithi sio hali ya hewa tu bali na uchumi wake. Kitu mnachoongea leo kinaenda sambamba na kauli mbiu ya mkoa ambayo inasema ‘Dodoma, fahari ya Watanzania’. Tayari Serikali ya awamu ya sita  imetoa Tsh.221.0 bln kwa ajili ya kuhakikisha umeme unafika kila mahali Dodoma. Hivyo viongozi wa dini tuwekeze Dodoma . Fursa bado ni nyingi, bado tunahitaji hotel na kumbi za kisasa, huduma za afya,huduma za kimataifa na maeneo ya starehe ( recreational centre). Dodoma ni pamoja na Wilaya zake zote Saba”. Amesema Senyamule.

Aidha, Mkuu wa Mkoa amewatangazia fursa za uwekezaji zinazopatikana Dodoma, kwani kuna maeneo ya kutosha na watu mbalimbali wanakuja kuomba kuwekeza hapa hivyo kama kanisa lina nafasi linaweza kuitumia au kuitangaza kwa ajili ya uwekezaji. “Watu wanatoka kila nchi na kila mahali kuja kuwekeza Dodoma, fursa zipo nyingi. Nitoe wito kwa Kanisa na Viongozi wa dini, tuwekeze Dodoma” Ameongeza

Naye Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanganyika,  Askofu Dickson Chilongani, amesema kuwa Kanisa lake linafanya uwekezaji katika kilimo pamoja na kuunga mkono kauli mbiu ya kuifanya Dodoma ya kijani kwa kufanya kampeni ya kupanda miti.

“Tumehamasisha kila Parish iwekeze katika majengo bora, kilimo cha Alizeti, Zabibu na Korosho  pia tunajihusisha na kauli mbiu ya kuifanya Dodoma ya kijani kwa kugawa miche 1000 ya miti kwa kila Parish .Tunataka kwenye kila  Parishi zetu 300, kila Parishi iwe imepanda miti 1000 hivyo baada ya muda tuwe na jumla ya miti 300,000.”  Amesema Askofu Chilongani.

Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanganyika, limeandaa warsha ya siku tatu iliyoanza tarehe 11 Oktoba na inatarajiwa kutamatika tarehe 13 Oktoba. Warsha hii inashirikisha Makasisi wote wa Dayosisi ya kanda ya kati  lengo kuu ni kujadili namna kanisa linavyojihusisha na masuala ya kiuchumi.Kauli mbiu ya Warsha hiyo ikiwa  ‘Kanisa  na uwekezaji’. MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.