• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC SENYAMULE KUDILI NA WATAKA RUSHWA

Imetumwa : February 11th, 2024

Suala la kuongea, kusikiliza na kutatua kero  za makundi mbalimbali ya wakazi wa Jiji la Dodoma wakiwemo wafanyabiashara, madereva boda boda, wachimba madini n.k limekua endelevu kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule na lenye matokeo chanya na muitikio mkubwa kwa makundi husika.

Februari 11/2024 katika ukumbi wa New Generation- Kisasa  katika semina ya siku moja ni zamu ya Mafundi Ujenzi wa Mkoa wa Dodoma ambao nao wanapata wasaa wa kuteta na Mhe. Senyamule ambae anawahakikishia kupambana na wote wanaoleta vikwazo mbalimbali ikiwemo kuombwa rushwa pindi wanapoomba kujenga Miradi ya Serikali pale inapotangazwa licha ya kukidhi vigezo muhimu.

"Naomba niwahakikishie kuwa tunaendelea kushughulika na wote wasio na dhamira njema na Mhe. Rais ya kutamani nyie mfanye kazi za Ujenzi wa Miradi ya Serikali bila kikwazo pale mnapokidhi vigezo, namba zetu mnazo mkikutana na vikwazo vya rushwa wakati mnaomba kazi tutumieni meseji na sisi tutashughulika nalo kwa haraka sana", ameahidi Senyamule

Hata hivyo kumekua na baadhi ya Mafundi wasio waaminifu wanaoshindwa kuwalipa Mafundi wasaidizi kwa wakati licha ya wao kulipwa na Serikali Stahiki zao, Mhe. Senyamule amebaini tatizo Hilo na kuwataka Mafundi kuwa na utu na kuzingatia makubaliano waliyojiwekea ili kufanya kazi kwa ufanisi unaotakiwa.

"Wapo Mafundi ambao hawawalipi vibarua wao kwa wakati na hiyo ni changamoto tumekutana nayo katika baadhi ya maeneo, licha ya kwamba wao wameshapokea Fedha kutoka serikalini sasa Kama mnavojua mtu asipolipwa stahiki zake anakua na ugumu na kazi zinakua zinafanyika kwa kusua sua sasa walipeni wenzenu ili kazi zifanyike kwa haraka na ufanisi mkubwa Kama ulivyotarajiwa", amesema Senyamule.

Aidha  Mhe. Senyamule ametoa wito kwa mafundi ambao hawajajiunga na Chama Cha mafundi rangi na Ujenzi (CHAMARAUTA) kujiunga na chama hicho kwani Kuna tija kubwa ya kuwa na chama hicho hususani katika kujipatia kazi na vitu vingine vya msingi katika kazi yao

Akizungumza kwa niaba ya wengine Mkurugenzi wa RockMax international Limited Hamoud Abdallah amesema  takribani  mafundi 1,000 wa Mkoa wa Dodoma  walioajiriwa na waliojiajiri ikiwemo mafundi wa Serikali na kutoka sekta mbalimbali wamehudhuria semina hiyo.

"Mafundi waliohudhuria hapa ni takribani mafundi 1000 na hii ni matumaini ya kwamba wataenda kuwa mabalozi wazuri na kufundisha wengine huko katika maeneo yao

 ya Kazi", amesema Abdalla 

RockMax International Limited ambao ni watengenezaji wa bidhaa mbalimbali za Ujenzi hususani extra power skimming putty ndio walioendesha semina hiyo ya siku moja , Februari 11,2024 kwa mafundi hiyo.













ReplyForward


Add reaction










Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.