• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC SENYAMULE,Akagua Mradi wa Kituo cha Afya na Mradi wa Maji Kijiji cha Mkoka, Kongwa ataoa Maelekezo

Imetumwa : September 1st, 2022

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Staki Senyamula hivi karibuni  amefanya ziara Wilayani Kongwa na kutembelea  mradi wa maji na mradi wa kituo cha afya  vilivyopo kata ya Mkoka.

Akizungumza mkuu wa wilaya ya Kongwa Mhe. Remidius Mwema Emmanuel amesema Wilaya ya Kongwa ni eneo la kihistoria kwani wapigania uhuru wengi wa nchi za kusini mwa Afrika  waliishi Kongwa.Hivyo Wilaya ya kongwa imekuwa ikipata wageni wengi ambao wamekuwa wakija kutembelea eneo hilo la kihistoria na hivyo kuifanya Wilaya hiyo kuwa na mkakati wa kuboresha maeneo ya kihostoria na hatimae hapo  baadae kuja kuwa vyanzo vya mapato.

Akitoa taarifa ya Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Kongwa Dkt. Omary Nkullo amemueleza mkuu wa mkoa kuwa ujenzi wa mdarasa ya UVIKO umekalimika, na kwa kutumia fedha hizo hizo wameweza kujenga na kuanzisha shule mpya saba.Dkt. Nkullo amemweleza mkuu wa mkoa kuwa wanaendelea na zoezi la kuvisha ng’ombe hereni,na miradi ya afya iliyofadhiliwa na Serikali ya Korea pamoja na mradi wa kudhibiti sumu kuvu, mradi wenye thamani ya Tsh 99bln katika eneo la  mtanana ambao bado unaendelea,  Mradi huo unapatikana  kongwa tu nchi Tanzania .

Katibu Tawala Mkoa wa Dododma Dkt. Fatuma Mganga, amewapongeza  Kongwa kwa ukusanyaji wa mapato na kusema kuwa Kongwa inafuatia halmashauri ya  jiji la Dododma kwa ukusanyaji wa mapato. Pamoja na ukusanyaji huo, halmashauri ya Kongwa bado wanachangamoto kubwa sana ya watoto kuacha shule, watoto 4419 wameacha shule wakiwa darasa la nne.Kwa upande wa Sekondari 26% ya wanafunzi ni Watoro,kidato cha nne wanafunzi 492 sawa na 11.3% hawajafanya  mtihani wa mock.

“Tuna mradi wa shule bora na msaada wao unategemea jinsi wanafunzi wanaongia darasa la kwanza na kumaliza darasa la saba (rentation rate), hivyo waalimu na wazazi tusipozuia hili tutakuwa tunakosa misaada kama hii. Wito wangu Watoto watoro wasakwe kwa kampeni kubwa na warudishwe shule kwani Mhe.Rais alishatoa kibali cha watoto waliocha shule kurudishwa mashuleni”.Amesisitiza Dkt. Mganga.

Akizungumzia nia na malengo ya ziara yake Wilayani Kongwa,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Senyamule amesema ziara yake Wilayani Kongwa ina lengo  la kujitambulisha, kukagua miradi na kutoa Maelekezo.

Mkuu wa Mkoa amewapongeza Kongwa kwa kazi nzuri ya Sensa na Mwenge.Tuweke mkazo na tuliongezee nguvu na tuwaelimishe wananchi umuhimu  wa kuwavalisha hereni mifugo yetu.Kuhusu masula ya wananchi kuandikisha kwa ajili ya ruzuku ya mbolea na msuala ya kilimo ni vyema wananchi wakaelezwa umuhimu wa kutumia majina yaliyopo kwenye kitambulisho cha NIDA na Wapiga kura kwani hii itapunguza changamoto ya utofauti wa majina .Royal Tour inafaa sana Dodoma.Kuna vitu vingi vinapatikana Dodoma na havipo mikoa mingine hivyo ni vyema tukatumia fursa hizo kwa ufasaha.

Akiwa Wilayani Kongwa, Mkuu wa Mkoa ametembelea mradi wa Kituo cha afya na mradi wa maji, miradi ambayo bado inaendelea na utekelezaji.  Kituo cha afya Mkoka kilipokea jumla ya  Tsh. 300mln katika mwaka wa fedha 2021/2022 kwa ajili ya kujenga majengo ya kujifungulia/wazazi, upasuaji na maa ara. 97% ya jengo la wazazi na jengo la upasuaji imekamilika, ujenzi wa maabara utakamilishwa awamu nyingine ya fedha. Pamoja na ukamilishaji huo mradi u mekuwa ukikabidliana na changamoto ya mfumuko wa bei na hivyo wazabuni kukataa kuleta vifaa. Mradi huo umewanufaisha wananchi kwani umezalisha ajira zaidi 60 na kuongeza kipato kwa mama lishe/ wauza chakula.aidha mtradi huo umepunguza adha ya kusafiri wa kilometa zipatazo 45  za kwenda kufuata huduma ya afya na hivyo kupunguza gharama za usafiri.

Akizungumzia Mraji wa Maji wa kijiji cha Mkoka ,Mhandishi Jumanne Selemani- kutoka Mashauri trading coy, amemweleza Mkuu wa Mkoa kuwa mradi huo ni wenye thamani ya Tsh.681.5 mln, tayari wamesha jenga pumpu house,na kuweka tanki lenye ujazo wa   50,000 lts, Ujenzi wa kisima chenye  urefu. 20.3m na ulazaji wa mabomba unaendelea, vile vile wamejipanga kukarabati tenki la zamani ili litumike. Ukarabati huo utawanufaisha wananchi 10918 pamoja na mifugo yao kupata maji.

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa hiyo. Mkuu wa mkoa wa  Dodoma Mhe. Senyamule amesema lengo la miradi hii ni kuwafikishia kwa urahisi huduma ya afya wanakijiji Cha mkoka huduma ambayo walikuwa wanatembea umbali wa Km 45 ili kufuata huduma hiyo. Ujenzi wa jengo la kina mama (Kujifungulia naupasuaji) itawasaidia wananchi wa Mkoka kupata huduma na kuwafikia kwa ukaribu na hivyo kuweza kupunguza vifo visivyotarajiwa. Akizungumzia umuhimu wa miradi, Mhe. Senyamula amesema kila mwanakijiji anapaswa kujua na kuangalia mradi wao unaendelea. Kila  mtu analo jukumu la kuangalia hii miradi, nimekuja kuangalia matumizi za fedha ya miradi na ubora ya majengo yaliogengwa.

Aidha Mhe. Senyamule Ametoa  wito kwa mkurugenzi  kuweza kutekeleza na kuendelea na maboresho hayo ili ifikapo Oktoba 1 mwaka huu wanakijiji wa Mkoka ,waweze kupata huduma hii na wakina mama waweze kujifungulia katika hospitali hii ili dhamira wa Rais wetu Mhe Samia Hassan Suluhu  iweze kutimia."Dhamira ya Serikali yetu ni kupunguza vifo vya wakina mama wakati wa kujifungua kama wakina mama mlikuwa na njia nyingine ya kujifungulia Sasa huduma inakuja karibu yenu ili lengo la Serikali yetu ni kuondoa na kupunguza  vifo vya mama na mtoto, Vifo vya uzembe wa kutokwenda hospitali ni Vifo vya kujitakia ambayo Serikali haivitaki. Kama Vifo vikitokea basi viwe vile ambayo Mungu ameviruhusu yaani vya mapenzi ya mungu.Hapa  mtapata huduma nzuri na vifaa vitakuwepo vya kutosha”. Amesisitiza RC-Senyamule

Aidha Mkuu wa Mkoa  amewasihii wakina baba kuungana na wake zao wanapoenda Kliniki  na  kuwakumbusha kufika hospitali wiki moja kabla ya kujifungua ili kupata ushauri wa kitaalam utakao okoa uhai wa Mama na Mtoto.

Kuhusu Mradi wa Maji Mkuu wa Mkoa amemtaka mkandarasi na wanakijiji cha Mkoka kulima miti ambayo ni rafiki na maji.Ili maji yadumu,lazima yatunzwe, kwenye kila chanzo cha maji lazima kupandwe miti ambayo ni rafiki ya maji  na hili lifanyike kabla ya mwisho wa mwezi wa Tisa/ Septemba , ili  maji yasikauke bali yasongezeke. Mwisho.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.