• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RUSHWA YA NGONO KWENYE VYUO VIKUU/ELIMU YA JUU NI HATARI KWA MSTAKABALI WA MAENDELEO YA KWELI YA NCHI

Imetumwa : June 21st, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge ameitaka Taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa TAKUKURU Mkoani Dodoma kwa kushirikiana na uongozi wa vyuo vikuu, elimu ya juu na klabu za kupinga Rushwa vyuoni kuhakikisha wanakomesha vitendo vya Rushwa ya ngono vyuoni. 

 

Dkt. Mahenge ametoa agizo hilo mwishoni mwa wiki wakati akifungua mafunzo ya siku moja ya kupambana na Rushwa ya ngono vyuoni kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na elimu ya juu Mkoni Dodoma yaliyofanyika katika chuo cha mipango ya maendeleo vijijini ambayo yameendeshwa na TAKUKURU Mkoani Dodoma ambapo alibainisha kuwa Rushwa ya ngono vyuoni ina madhara makubwa kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

Amesema kuwa Rushwa ya ngono vyuoni inasababisha kuporomoka kwa Elimu na kuporomoka kwa sifa ya taaluma ya vyuo vikuu na Elimu ya juu. Dkt. Mahenge ametaja baadhi ya madhara yanayosababishwa na Rushwa ya ngono vyuoni kuwa ni pamoja na kuanguka kwa Elimu na maadili, kupatikana kwa wasomi wenye uwezo Duni wasiokuwa na sifa stahiki, wasomi kupata vyeti wasivyostahili.

Ameongeza athari zingine ni kuajiriwa watu wasiokuwa na sifa na utendaji kazi kuanguka makazini, mahusiano mabaya makazini, kuongezeka kwa magonjwa ya zinaa na UKIMWI, ongezeko la mimba zisizotarajiwa, ukiukwaji wa haki za binadamu na utawala bora.

Kufuatia athari hizo, ameitaka TAKUKURU kwa kushirikiana na uongozi wa vyuo vikuu na Elimu ya juu na Klabu za kupambana na Rushwa vyuoni kuweka mikakati ya pamoja ya kupambana na tatizo hili na kuhakikisha vyuo vinaweka sheria ndogo zenye kusimamia maadili kikamilifu.

Katika hatua nyingine, Dr. Mahenge amewaonya baadhi ya wanafunzi wa kike wa vyuo vikuu na vyuo vya Elimu ya juu Mkoani Dodoma wenye tabia za kutumia miili yao kama kishawishi cha kuwatega kingono Wahadhiri wa kiume kwa lengo la kusaidiwa kupata alama nzuri na kufaulu masomo/mitihani yao. 

 

Nae Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Bw. Sosteness Kibwengo amesema kuwa kuna ongezeko la malalamiko ya Rushwa yasiyo rasmi katika vyuo lakini taarifa rasmi zinazofikishwa TAKUKURU ni chache .

 

Ametaja kuwa tafiti iliyofanywa na TAKUKURU miezi ya mwanzoni mwa mwaka huu wa 2020 imeonesha kuwa asilimia 68% ya Watumishi wa vyuo na asilimia 57% ya wanafunzi wa vyuo walioulizwa katika utafiti huo walikiri kuwa bado kuna Rushwa ya ngono katika vyuo.

 

Kwa upande wa maoni ya wanafunzi wa vyuo, Kijana Amos Mgidange mwanafunzi wa chuo cha mipango ya maendeleo Vijijini - IRDP alisema kuwa, tatizo la Rushwa ya ngono vyuoni lipo na wakati mwingine lipo hata kwa wanafunzi wa kiume ambapo baadhi ya wahadhiri wa kike wamekuwa wakiwataka kingono wanafunzi wa kuime vyuoni.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.