• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SENYAMULE AAGIZA UJENZI WA MADARASA KUKAMILIKA KWA WAKATI

Imetumwa : May 29th, 2023


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule leo Mei 29, 2023 ameendelea na ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mabweni katika Shule ya wasichana Bunge, ujenzi wa Shule mpya ya msingi katika eneo la Swaswa na madarasa ya awali katika Shule ya msingi Kisasa ambapo ujenzi wake uko katika hatua za ukamilishaji.

Katika kaguzi hizo Mhe. Senyamule ametoa maagizo kwa wasimamizi wa mradi kuhakikisha kazi inakamilika kwa muda uliopangwa na kuzingatia viwango vya ubora huku akitoa rai kwa wasimamizi wa ujenzi kukaa na mafundi ili kufanikisha ukamilishaji wake.

“Mkoa wa Dodoma tumejipanga kukamilisha hizi kazi kwa wakati hivyo wataalamu mkae na mafundi mpitie kwa pamoja mpango kazi wa miradi hii ili tujue kila siku ni kazi gani inatakiwa kukamilika kwa siku husika ili itakapofika tarehe 15 Juni 2023 ujenzi uwe umekamilika” Senyamule amesisitiza.

Aidha, Senyamule amesema kuwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa fedha zote kwa wakati hivyo hakuna sababu za kuchelewa kufanya manunuzi. Amesema ni wajibu wa wataalamu kuhakikisha ununuzi wa vifaa vyote vinavyohitajika vinapatikana ili mradi uweze kukamilika kwa muda uliopangwa.

Mkoa wa Dodoma kupitia mradi wa Boost umepokea kiasi cha Shilingi Bilioni 10.6 kwa ajili ujenzi wa Shule mpya 16, vyumba vya madasa ya msingi 163, madarasa ya awali 16, ujenzi wa vyoo 106, nyumba za walimu 03 na darasa 01 la elimu maalumu.

Shule ya Msingi Kisasa imepokea kiasi cha Shilingi Milioni 63.6 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 2 na vyoo 6 huku Shule ya Swaswa imepokea kiasi cha Shilingi Milioni 318.8 kwa ajili ya kujenga Shule mpya itakayokuwa na madarasa ya msingi 7, madarasa ya awali 2 na Vyoo 12.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.