• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SENYAMULE ATOA SIKU TATU WAKAZI WOTE WA KATA YA HAUBI WALIO TOA ANUANI ZA MAKAZI KUZIRUDISHA

Imetumwa : September 16th, 2023











Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ametoa siku tatu (3) kwa wakazi wa Kata ya Haubi iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kuhakikisha wanarudisha anuani za Makazi zilizo wekwa na serikali kama sehemu ya utambulisho  kwa Wananchi wote waliotoa huku akiwahakikishia  hatua za kisheria zitachukuliwa kwa watakaoenda kinyume na maelekezo hayo.

Kauli hiyo imetolewa Septemba 15,2023 wakati wa ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa ya kukagua miradi ya maendeleo na miundombinu mbalimbali katika shule mpya ya Sekondari katika Kata ya Bolisa, Shule mpya ya Sekondari Ntomoko iliyopo katika Kata ya Haubi sambamba na kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Kata ya Haubi, Ujenzi huo unatekelezwa kupitia Fedha za SEQUIP

"Kawatangazieni na wengine tunatoa siku tatu kwa yeyote aliyetoa anuani za Makazi ahakikishe anarudisha sehemu husika alipotoa kwa asiyerudisha tutamfungulia mashitaka "amesisitiza Senyamule

Aidha, Kiasi cha zaidi  ya shilingi  Millioni 544 zimewekwa kwenye account ya  Shule ya Sekondari Hubali kwa ajili ya Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Bolisa unaohusisha Jengo moja la Utawala, Vyumba nane vya madarasa, matundu nane ya vyoo vya wanafunzi, Jengo moja la Maktaba, Jengo moja la Tehama pamoja na  majengo matatu ya maabara 

Pia, Katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ilipokea kiasi cha zaidi ya shilingi Millioni 544 kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Ntomoko iliyopo katika Kata ya Haubi, mradi ambao unahusisha ujenzi wa Jengo moja la Utawala, Jengo moja la Tehema, Vyumba viwili vya madarasa na Ofisi moja, katika (BLOCK A na B ), Vyumba viwili vya madarasa (BLOCK C na D), Ujenzi wa madarasa matatu ,Jengo la Maktaba, matundu nane ya vyoo, kichomea taka ,chumba cha mahitaji maalum pamoja na tenki la maji ya ardhini.

Mhe.Senyamule amehimiza suala la Usalama wakati akijibu changamoto mbalimbali za wananchi wa Kata ya Haubi amewataka wazazi na walezi kusimamia malezi ya watoto wao ili kulinda mila na tamaduni pamoja na maadili ya  taifa.

"Suala la Usalama linaanza na sisi, tuanze wote kwa pamoja kwa kuchukua hatua za kusimamia malezi mazuri ili nchi yetu  isiwe na watoto wabakaji, walawiti, wavuta bangi na mmomonyoko wa maadili "Amesisitiza Senyamule

Mkuu wa Mkoa huyo amewaasa vijana na watu wote wanaojishughulisha na kilimo na biashara ya bangi  kuacha mara moja kwani ni kinyume na taratibu za nchini ya Tanzania na kuwaagiza kuhakikisha kila mmoja anakuwa mlinzi wa mwenzake kwa kukemea na kutoa taarifa kwenye vyombo vya sheria.

"Natoa shime mnajua bangi ni kinyume cha sheria na taratibu wengine tayari wapo ndani, kama kuna watu bado  wanaweka bangi ndani watumieni salamu, hatutaki vijana wetu waharibikiwe kama kuna wanaolima tuwakemee kwahiyo lazima kila mtu awe mlinzi wa mwenzake. "Amesisitiza Mhe.Senyamule

Kwa Upande Wake, Diwani wa Kata ya Haubi  Mhe. Paulo Raymond amemshukuru Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ujenzi wa Shule mpya ya Ntomoko kwani itawasaidia watoto kutotembea umbali mrefu kufuata elimu pamoja jitihada mbalimbali zenye manufaa kwa Wananchi wa nchi ya Tanzania. 

Aidha, Katika ziara hiyo Mhe.Senyamule amefanikiwa kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili wananchi wa Kata ya Haubi na baadhi amezichukua kwa ajili ya utekelezaji na hivyo amewahimiza wananchi kuendeleza Amani na kushirikiano kwa serikali popote wanapohitajika kutoa usaidizi wao.
























Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.