• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SENYAMULE AZINDUA JUKWAA LA PILI LA VYAMA VYA USHIRIKA

Imetumwa : May 19th, 2023


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amezindua jukwaa la pili la Maendeleo ya Vyama vya Ushirika  Mkoa wa Dodoma lenye dhamira ya kuinua uchumi wa vyama mbalimbali vya kifedha (SACCOS) na kukuza uchumi wa wakulima wa mazao ya kibiashara na kimkakati. Uzinduzi huo umefanyika hii leo tarehe 19/05/2023 katika viwanja vya Nyerere square jijini.

Akizindua jukwaa hilo Senyamule amesema vyama vya ushirika ni njia ya kuinua uchumi kwa haraka vile vile ni njia inayotoa fursa za uwekezaji na ajira.

"Vyama vya ushirika ni njia rahisi ya kujenga uchumi kwa haraka na sisi kama Serikali tuko tayari kuviwezesha vyama hivi vile vyenye nia ya dhati ya kushirikiana, wenyenia tutawainua na mtawaona watakuwa mfano wa kuigwa,Tumieni fursa zinazopatikana vizuri " Amesema Senyamule

Aidha Mhe. Senyamule amevitaka vyama hivyo viendelee kukua kwa kuongeza Idadi ya wanachama, hisa, amana, mitaji na uwekezaji vitu ambavyo vitawafanya kukua kiuchumi na kukuza uchumi wa Dodoma na Taifa kwa ujumla.

Kwa Upande wake Mrajisi na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) Dkt. Benson Ndiege amewataka wanachama wote wa vyama vya ushirika Mkoa wa Dodoma kujisajiri rasmi Hadi kufikia Mei 30 mwaka huu ambapo zoezi la usajiri litafikia kikomo.

Naye Kaimu Mrajisi Msaidizi Mkoa wa Dodoma Bw. Octavian Bidyanguze amesema vyama vya ushirika vimekuwa mstari wa mbele katika kutoa ajira kwa vijana wa kitanzania na kupunguza tatizo la ajira nchini kwani hadi sasa wamefanikiwa kuajiri watumishi 110 katika sekta tofauti kwa ajira za kudumu na mikataba ya muda mfupi.

Mkoa huo unajumla ya vyama vya ushirika 124 ambavyo vyama vya SACCOS ni 57,vyama vya kilimo na masoko AMCOS 49 na vyama vingine 18 ambapo jumla ya wanachama ni 11,359 kati yao wanawake ni 5,112 na wanaume 6,012 na jumla ya vikundi 235.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.