• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SENYAMULE AZINDUA KITUO JUMUISHI CHA MANUSURA WA UKATILI

Imetumwa : January 27th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amezindua kituo cha utoaji huduma jumuishi kwa manusura wa ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto kilichopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Akizindua kituo hicho Mhe. Senyamule amesema Mradi wa USAID Afya Yangu umekuja kwa wakati muafaka kwani Mkoa wa Dodoma ni kati ya Mikoa yenye changamoto za matukio ya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya Watoto, hivyo kituo hicho cha kwanza katika Mkoa kitasaidia manusura wa ukatili ambao watapata huduma zote kwa haraka kwa wakati muafaka.

“Jengo hili la kutolea huduma jumuishi kwa manusura wa vitendo vya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto ambalo ninalizindua leo ni moja ya malengo ya mpango jumuishi wa utoaji huduma kwa manusura wa vitendo vya ukatili uliozinduliwa mnamo mwaka 2013. Lengo la kuanzishwa vituo hivi ni kuhakikisha huduma  zinatolewa kwa manusura wa vitendo vya ukatili kwa uharaka na kwa uratibu mzuri pia kurahisisha mfumo wa rufaa kwa manusura katika kupata huduma maalum zingine kama vile msaada wa kisheria” Alisisitiza Mhe. Senyamule

Manusura wa vitendo vya ukatili wamekuwa wakipata changamoto katika kupata huduma kwa uharaka na kwa uratibu mzuri kutokana na mtawanyiko wa maeneo ya huduma muhimu wanazozihitaji ikiwemo huduma za afya, Ustawi wa Jamii na huduma za kisheria. Hali hii imesababisha baadhi ya manusura kukosa huduma kwa wakati na kupata madhara yakiwemo maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, Ulemavu wa kudumu, mimba zisizotarajiwa na mimba za utotoni zaidi kutokana na vitendo vya ukatili walivyofanyiwa.

“Uwepo wa kituo hiki cha utoaji huduma jumuishi katika Mkoa wa Dodoma utawawezesha manusura wa vitendo vya ukatili kupata huduma kwa uharaka na kwa uratibu mzuri na mwisho kuwawezesha kupata haki zao katika vyombo vya sheria” Amesisitiza Mhe. Senyamule.

Mhe. Senyamule amempongeza Bw. Chip Lyons Rais wa shirika la EGPAF kupitia “mradi wa Afya Yangu” kwa kusaidia ukarabati wa jingo la kituo hicho pamoja na kuwezesha upatikanaji wa vifaa kwa ajili ya kuanza kutoa huduma.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.